Tuesday 1 March 2016

KUFUATIA TAMKO LAKE KUTAKA WALIMU WA WILAYA YA KINONDONI KUPANDA DALADALA BURE MAPYA YAIBUKA.


                      Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Paul Makonda.

Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Paul Makonda kutangaza kuwa Walimu wa shule za Dar es salaam kuanza kupanda daladala bure baada ya kukubaliana na wamiliki pamoja na madereva wa daladala, watu mbalimbali wamekuwa na  maoni tofauti huku wengi wakimkosoa.


Na hivyo makonda ajibu kwa kusema haya,
 ‘Najua nipo kwenye jamii ambayo inapenda kuongea sana kuliko kufanya kazi, jamii inayojua kuongelea kukwama kwa jambo hata kabla ya kuanza kufanya kazi 

Watu wengi wanesema tungewapa pesa ya nauli, wengine wanasema pesa hizi wangepewa wanafunzi, wanasahau kama Walimu ndio uti wa mgongo wa taifa


Huu ni mchabgo wa wadau, wadau ndio wanawasaidia Walimu, mimi nasimama kama daraja na kufikisha kilio kwa wadau, watu wasichanganye mambo, Mkuu wa Wilaya hana pesa..wao wamepewa usafiri‘Alisema Makonda.

No comments:

Post a Comment