Thursday 17 March 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA WATATU WA SERIKALI WILAYANI CHATO.




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Chato.

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Kassimu Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watatu wa Serikali wilayani  Chato kwa makosa tofauti ikiwemo ya ubadhilifu wa fedha ,na madai ya fedha kwa sakosi mbili ambazo alikuwa akidaiwa  Afisa ushirika ikiwa ni pamoja na kuuwa ushirika wa sakosi ya umoja.


Waliosimamishwa   ni mhandisi wa maji Peter Ngolemo  kwa tuhuma za kupotea kwa pampu katika kijiji cha Karebezo Kata ya Mirembe, Warioba Mwita ambae ni Afisa Ishirika kwa  kile kinachodaiwa kuwa alikopa  fedha katika sakosi na kushindwa kurejesha fedha  hali  iliyopelekea kuwepo kwa migogoro katika  sakosi  mbili ya walimu na umoja,na  Afisa maendeleo ya jamii  pamoja na Dionizi Mulayoba  kosa lake ni ubatilifu wa fedha..

Aidha waziri Majaliwa amewataka watumishi wa serikali kubadilika na kuhakikisha  wanafuata misingi ya uadilifu pindi wawapo kazini ikiwa ni pamoja na kuwa wawajibikaji katika maeneo ambayo wanatakiwa kujituma kwa bidii zaidi ili kuleta maendeleo kwa nchi na kwamba hakuna mtu yeyote  atakaye lindwa endapo  akienda kinyume na kanuni na sheria ya nchi katika swala la uwajibikaji.


Waziri mkuu leo anatarajia kumaliza ziara yake ya kikazi mkoani hapa kwa kukutana na viongozi wa ngazi mbali mbali  ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi wa Katoro wilayani Geita.

No comments:

Post a Comment