Shirika la Afya Duniani (WHO)
limesema uvutaji wa sigara unabaki kuwa chanzo kikuu cha vifo ambavyo
vingeepukika licha ya kupungua kwa matumizi ya sigara duniani tangu kuanza kwa
karne ya 21.
KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Thursday 31 May 2018
"WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA" – PM MAJALIWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipowasili
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuzindua Maadhisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31,
2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Kate Kamba wakati
alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kuzindua Wiki
ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dkt. Hamisi Kigwangalla na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhandisi
Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw.
Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutokana na takataka na kufungashwa
kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo
kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam, Mei 31, 2018. katikati ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space
Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutoka na
takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea
banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa
Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo,
Neema Matemba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabada ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi
Nimwagile Mwaijumba wakati alipotembelea banda la Kituo cha Utengenezaji magari
cha Nyumbu na kujionea mashine ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia
takataka iliyobuniwa na kutengenezwa na kituo hicho. Waziri Mkuu alitembelea
mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na wapili
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Opwani Mhandisi, Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza
Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David Mwendapole wakati alipotoa maelezo
kuhusu majiko makubwa yanayotumia gesi kidogo katika maonyesho ya
Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31,
2018. Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika
maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei
31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi
baada ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam, Mei 30, 2018. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarest Ndikilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala,
Mwenyekiti wa CC wa Mkoa wa Dar es alaam, Kate Kamba,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,
Kisare Matiku Makori na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira, January Makamba.
SERIKALI KUENDELEA KUCHUKUA HATUA ZA KISERA KUHAKIKISHA RIBA ZA MIKOPO ZINAPUNGUA
Waziri wa Madini Mhe. Angellah
Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya
Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge
Uratibu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa
maelezo Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika
kuwalinda watoto wa kike ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa taarifa rasmi
kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowadhalilisha kijinsia watoto wa kike
na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na
Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI
hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue hali zao na kuchukua hatua
stahiki.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali
Venance Mabeyo (wakwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe
Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula
aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim
Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Sehemu ya Viongozi wa Tume ya Madini na wageni
mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini wakifuatilia hotuba ya
Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo.
Sehemu
ya Wanafunzi waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa
Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Tuesday 29 May 2018
WAZAZI WATAKIWA KUACHA KUWAAGIZA WATOTO MAENEO YA MGODI WA GGM
Watoto wakiwa kwenye shimo la kutupia uchafu
ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)wakiogota vyuma chakavu vinavyokuwa
vimetupwa na mgodi huo.
Afisa mahusiano wa mgodi wa GGM Mussa Shunashu akionesha maeneo ambayo ni hatarishi kwenye mgodi huo.
Eneo la kutupia taka kwenye mgodi wa dhahabu wa
Geita.
Bi. Sarah Kajoro akiwa kwenye masikitiko
kutokana na mtoto wake kushindikana na kujikuta akielekea maeneo ya mgodini.
Mzazi akijaribu kumwazibu mwanae kutokana na
kuwa na tabia ya kwenda kwenye maeneo ya mgodi wa GGM.
|
Mwenyekiti wa mtaa wa Kompaundi Edgha Onyango
akielezea hatua ambazo wameendelea kuzichukua dhidi ya wazazi ambao wamekuwa
wakiwaruhusu watoto wao kwenda maeneo ya mgodini.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi
akikemea vikali tabia ya baadhi ya wazazi kuendelea kuwatumikisha watoto kuwa
watafutaji badala ya wao kutafuta.
|
WAVUVI KATA YA NKOME WALALAMIKIA KUONEWA NA WATU KUTOKA IDARA YA UVUVI
Wavuvi wa
mwalo wa Makatani kata ya Nkome wilayani Geita wakiendelea na maandalizi
kwaajili ya kwenda kwenye shughuli ya uvuaji wa dagaa.
Zana za uvuvi ambazo wamelalamikiwa kuwa
zinakamatwa na maafisa uvuvi kwa madai kuwa zinashiriki kwenye suala la uvuvi
haramu.
|
Mzee Yohana Kulwa akielezea masikitiko yake
kutokana na suala kuendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya
uvuvi bila ya kuwa na makosa yoyote.
|
Wavuvi wa Mwalo wa
makatani Kata ya nkome Wilaya na Mkoa wa Geita,wamelalamikia kuonewa na watu
kutoka idara ya uvuvi kutokana na kuendelea kuwakamata na kuwapiga faini
pasipokuwa na makosa yoyote hali ambayo imeendelea kuwatia hofu pindi
wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.
Hatua hiyo imekuja ni
kutokana na msako ambao unaendelea ziwa Viktoria wa kuwakamata watu ambao
wameendelea kujihusisha na shughuli za uvuvi haramu.
Wakizungumza na Mwaandishi wetu baadhi ya wavuvi hao wamesema kuwa pamoja na kuendelea kutii
sheria kwa kutumia zana za uvuvi ambazo zinakubalika kwa mujibu wa sheria bado
wameendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya uvuvi.
Mwenyekiti wa
kitongoji hicho Bi. Anna Peter na Mwenyekiti wa BMU Bw,Peter John wamedai
kutokushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya kukamata watu hao na kwamba
elimu bado ni tatizo kwa wavuvi wengi kutokujua ni zana zipi ambazo
zinatumika kwenye shughuli zao kutokana na kutokupewa elimu.
Hata hivyo kwa upande
wake diwani wa kata hiyo,Masumbuko Nsembe amesema malalamiko ya wavuvi hao
amekwisha kuyapeleka halmashauri na kwamba hadi sasa yanafanyiwa kazi.
Mtandao huu
umemtafuta Mkuu wa oparesheni hiyo,Bw Roman Mkenda kwa njia ya simu ambapo
amesema kuwa baadhi ya wavuvi wamekuwa wakikimbia pindi wanapowaona
hali ambayo inasababisha wao kujua kuwa ni mvuvi haramu na kwamba
suala la elimu wamekuwa wakilitoa pindi mtu anapoomba kibali cha kutaka kuwa
mvuvi.
DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.
Bashiru Ally akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC
wakati akiwasilisha Ripoti ya Uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi CCM kwa
wajumbe hao Ikulu jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akiimba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali
Mohamed Shein mara baada ya kukabidhiwa makabrasha yenye taarifa za uhakiki wa
mali za Chama hicho.
Wajumbe kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa
NEC wakishangilia wakati kikao hicho kilipokuwa kikiendelea Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.
Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote
waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.
Bashiru Ally kwenye meza kuu mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na
wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.
Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote
waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally wapili kutoka kulia kwenye meza kuu kupitishwa
na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa NEC hawaonekani pichani, kushoto
ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally
Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe mara baada ya
kikao cha NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Monday 28 May 2018
PICHA: WABUNGE WAKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA MH. BILAGO
Baadhi ya Wabunge
wakisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu
Marehemu Kasuku Bilago.
Awali mapema leo Naibu Spika, Tulia Akson aliahirisha Bunge kutokana na Msiba huo, Mh. Bilago alifariki May 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.
Subscribe to:
Posts (Atom)