Friday 18 March 2016

WATU 3 WAFIKISHWA KIZIMBANI KWA WIZI WA MAFUTA AINA YA DIZEL WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA.


Jeshi  la Polisi Wilayani Bukombe Mkoani Geita limemfikisha Mahakama ya wilaya Paul Stephen (28) mkazi wa majengo mjini Ushirombo na wenzake wawili kwa wizi wa mafuta ya Dizel  lita 320 zenye thamani ya sh.573,360  walizoiba machi 14  saa kumi  usiku mjini Ushirombo.


Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya Veronika Seleman,  mwendesha mashtaka wa Polisi Elias Mgobera alisema washtakiwa  wote watatu mnamo machi 14 majira ya saa kumi  usiku waliiba mafuta aina ya Diszel lita 120 zenye thamani ya Sh.195360 mali ya Mussa Sospiter wa Ushirombo  huku pia ikisadikika waliiba tena mafuta aina Dizel lita 200 zenye thamani ya Sh. 368,000  ambayo mali ya Godliver Kimaro.

Washtakiwa hao wamekana shtaka kwa pamoja na hakimu veronica Selemani amewarudisha lumande hadi april 13 mwaka huu kesi  hiyo itakapotajwa tena.


Katika hatua nyingine kesi hiyo ilipelekea ugomvi kati ya Askari polisi na Maafisa wa TAKUKURU  huku ikiwa ni  kitendo cha ajabu katika jamii kwani  mahusiano yao  kuharibika yaweza kushindwa kuleta ufanisi kwenye utendaji wa kazi.  

No comments:

Post a Comment