Saturday 30 July 2016

SERENGETI BOYS YAJIPIMA KWA MADAGASCAR LEO


TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa chini ya miaka 17 ya Madagascar leo Jumamosi Julai 30, 2016 itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa wa Madagascar.

Friday 29 July 2016

TAARIFA YA WIZARA YA AFYA KUHUSU KUVAMIWA KWA SHIRIKA LILILOKUWA LIKIGAWA VILAINISHI SHINYANGA

Wizara imepokea taarifa kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Shinyanga imevamia ofisi za shirika la Jhpiego mkoani humo na kukamata baadhi ya watumishi wake kwa madai ya shirika hilo kugawa mafuta maalumu yanayodhaniwa kutumiwa kuhamasisha ngono za jinsia moja. Baada ya taarifa hiyo wizara inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

Thursday 28 July 2016

RAIS MAGUFULI KUHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA JUMAPILI WILAYANI KAHAMA

Rais John Magufuli anatarajia kufanya ziara wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako atafanya mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

JOSEPH SENGA ALIYEPIGA PICHA ZA TUKIO LA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI DAUD MWANGOSI AFARIKI DUNIA




Simanzi yatanda siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumhukumu kifungo cha  miaka kumi na mitano Askari  aliyemuua Daudi Mwangosi. Tasnia ya habari yapata pigo,mpiga picha wa gazeti la Tanzania aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi,JOSEPH SENGA amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATUA MGODI WA NYAMHUNA UNAODAIWA KUTESA NA KUUA MTANZANIA MMOJA






Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba jana  amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi  na suala kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro mkoani Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni watanzania.

PICHA:KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KILICHOPO NZEGA MKOANI TABORA







Tuesday 26 July 2016

MGOMO DALADALA WASOTESHA ABIRIA MWANZA

Mgomo wa mabasi ya kusafirisha abiria jijini Mwanza leo, umesababisha baadhi ya wakazi wa jiji hilo kutembea umbali mrefu kwa miguu na wengine kutumia usafiri wa vyombo vya usafiri visivyo salama.

WIZARA YA KILIMO YATANGAZA KUHAMIA DODOMA WIKI IJAYO


KATIKA kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kutaka serikali kuhamia Dodoma, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amesema watendaji wa wizara hiyo wataanza kuhamia Dodoma kuanzia wiki ijayo.

24 WAITWA STARS,MSUVA,JEBA,MNYATE NA MAHUNDI NDANI

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini Julai 31 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Nigeria unatarajiwa kuchezwa mwanzoni mwa mwezi Septemba.

YANGA NI YA KUJIPIGIA TU, INAPIGWA TU...NA LEO IMEPIGWA 3-1


YANGA SC imeendelea kuboronga katika mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo kufungwa mabao 3-1 na wenyeji Medeama FC Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi-Takoradi, Ghana.

WATANZANIA WAASWA KUWA WAMOJA KWENYE UJENZI WA NCHI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwaasa watanzania kudumisha amani ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa wetu kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili  Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Magufuli katika harakati za kuijenga Tanzania mpya.



Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa  Dkt.Ali Mohamedi Shein akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kusisitiza kuhusu umuhimu wa watanzania kuenzi amani iliyoasisiwa na wazee wetu na kuacha kushiriki katika vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.



Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Samweli Malechela akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kumshukuru kwa kusimamia na kutekeleza ahadi zilizowahi kutolewa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo kuhamishia serikali Mkoani Dodoma.



Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kumuahidi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa maagizo ya kuitaka Serikali ihamie mjini Dodoma.


Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa baada ya kuwekwa kwa silaha za asili za mashujaa na maua




Baadhi ya wananchi wakifuatilia shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiweka silaha za asili kwenye Mnara wa Mashujaa leo Mkoani Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania

Monday 25 July 2016

YANGA WAKAMUA SANA GHANA, KAZI WANAYO MEDEAMA KESHO

Yanga imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya Bohar mjini hapa kujiandaa na mchezo wa Jumanne dhidi ya wenyeji, Medeama ya Ghana.

SERENGETI BOYS KUELEKEA KAMBINI MADAGASCAR KESHO

Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, kikosi hicho kitaondoka kikiwa na wachezaji 19 viongozi wanne, Kiongozi mkuu Ayubu Nyenzi, kocha mkuu Bakary Shime, mshauri wa ufundi kwa soka la vijana Kim Poulsen,kit manager, na daktari wa timu.

WATANZANIA WAKUMBUSHWA KUWA WAZALENDO














Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema kuwa kufanyika kwa maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa inawakumbusha watanzania kuwa wazalendo.

Friday 22 July 2016

NAIBU WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO MHE. ANNASTAZIA WAMBURA AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA MZIKI TANZANIA



Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisini kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura kuwasilisha taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akizungumza na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime  mara baada ya  kupokea taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.



Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime akizungumza na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura ofisini kwa Naibu Waziri  wakati aki wasilisha taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
            



Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Habibu Msammy  akichangia mada wakati wa majadaliano kati ya  na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime  kuhusu maboresho ya tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akipokea  moja ya kazi ya muziki  wa dansi alizowahi kufanya Mzee Kitime baba wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.




Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime(kulia),  wa pili kushoto ni Afisa Utamaduni  kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Habibu Msammy  na kushoto katibu wa Naibu Waziri Bi. Anna Nkinda  leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.

KIKOSI CHA STARS DHIDI YA SUPER EAGLES KUTAJWA WIKI IJAYO


KOCHA Mkuu wa Tanzania, ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Jumanne ya Julai 26, 2016 anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

SAMATTA AFUNGA KWA PENALTI GENK YASONGA MBELE EUROPA LEAGUE





 Mbwana Samatta (kushoto) akiruka na kipa wa Buducnost

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ amefunga penalti ya tatu timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji  ikishinda kwa penalti 4-2 dhidi ya wenyeji Buducnost usiku huu Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica, Montenegro katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili ya mchujo wa kufuzu hatua ya makundi ya Europ League.
Timu hizo zilifikia kwenye matuta baada ya sare ya jumla ya 2-2, Genk ikianza kushinda 2-0, mabao ya Neeskens Kebano kwa penalti dakika ya 16 na Samatta dakika ya 79 Alhamisi iliyopita na usiku huu Buducnost wamelipa kisasi kwa ushindi wa 2-0, mabao ya Radomir Dalovic dakika ya 
kwanza na Milos Raickovic dakika ya 39.

Katika mikwaju ya penalti, mbali na Samatta wengine waliofunga upande wa Genk ni Thomas Buffel, Bryan Heynen na  Dries Wouters ya mwisho, wakati za Buducnost zilifungwa na Risto Radunovic  na Radomir Dalovic, huku Momcilo Raspopovic  na Luka Mirkovic  wakikosa.
Genk ilimaliza mchezo huo pungufu baada ya kungo wake Mghana, Bennard Yao Kumordzi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 75.

Sasa Genk itamenyana na mshindi wa mechi kati ya BK Hacken ya Sweden na Cork City FC ya Ireland katika Raundi ya Tatu, mechi ya kwanza ikichezwa Julai 28 nyumbani na marudiano Agosti 4 ugenini.
Mchezo wa kwanza baina ya BK Hacken na Cork City FC ulimalizika kwa satre ya 1-1 nchini Sweden. Ikumbukwe timu zitakazoshinda zitakwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi, ambako sasa vigogo kama Manchester United ya England wataanzia huko.
Kikosi cha FK Buducnost Podgorica kilikuwa: Dragojevic, Radunovic, Vukcevic, Vusurovic, Mitrovic, Vujovic/Hocko dk62 Raickovic, Raspopovic, Mirkovic, Janketic/Pejakovic dk52 na Dalovic.
KRC Genk: Bizot, Castagne, Dewaest, Kumordzi, Uronen, Ndidi, Buyens/Heynen dk45, Buffalo, Bailey, Karelis/Wouters dk74 na Samatta.


Thursday 21 July 2016

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI LA UKARABATI UWANJA WA NDEGE MJINI DODOMA


Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kutenga eneo la bandari kavu ili mkoa huo uweze kupokea na kuhifadhi mizigo na kurahisisha biashara kwa mikoa jirani.

Wednesday 20 July 2016

PLUIJM AONGEZA MIAKA MIWILI KUENDELEA NA KAZI YANGA SC


MHOLANZI, Hans van der Pluijm amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kufundisha klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

MBWANA SAMATTA AWANIA REKODI MPYA EUROPA LEAGUE LEO

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ leo anatarajiwa kuiongzoa timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili michuano ya Europ League dhidi ya wenyeji Buducnost nchini Montenegro.

SERIKALI KUENDELEA KUPAMBANA NA KUPINGA UTUMIKISHWAJI WA WATOTO NCHINI.



Mwakilishi wa Shirika la Watoto Duniani(UNICEF) Bi.Cecilia Baldeh akieleza jambo wakati  wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu ripoti ya matokeo utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akizungumza kabla hajazindua  matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akionyesha ripoti ya  matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mara baada ya kuizindua leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Kazi Dunia Tanzania Bw,Jealous Chirove.




Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akimkabidhi ripoti ya  matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani,Geneva Bw.Azfar Khan leo jijini Dar es Salaam

AJALI YASABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI MKOANI GEITA


Ajali  imetokea  jana majira ya saa tano za Asubuhi   katika eneo la Rukilini, Wilayani na Mkoani Geita na kusababisha watu 15 kujeruhiwa  huku mtu mmoja  akipoteza maisha  wakati akipatiwa   matibabu

MGONJWA AUWAWA MKOANI SINGIDA BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI WA TEZI DUME NA DAKTARI FEKI


Mkazi mmoja mkoani Singida anayedaiwa kuwa daktari feki anatuhumiwa kusababisha kifo cha mgonjwa, Israel Shabani (68) baada ya kumfanyia upasuaji wa tezi dume. 

Sunday 17 July 2016

JUMA ABDUL MCHEZAJI BORA, PLUIJM KOCHA BORA, HAJIB AMBWAGA TAMBWE BAO BORA

BEKI wa Yanga, Juma Abdul Jaffar Mnyamani ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.
Katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo usiku huu ukumbi wa Double Tree Hotel By Hilton, Masaki, Dar es Salaam, Abdul ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amewashinda beki mwenzake, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shizza Kichuya.
Na kwa ushindi huo, Abdul mbali na kukabidhiwa taji na mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, pia atazawadiwa fedha Sh Milioni 9.2 wakati klabu yake, Yanga SC itazawadiwa Sh. Milioni 81.3 kwa kuwa bingwa, huku Sh. Milioni 40.6 zikienda kwa washindi wa pili, Azam FC, Sh Milioni 29 zikienda kwa washindi wa tatu, Simba SC na Sh. Milioni 23.2 zikienda kwa Prisons washindi wa nne.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Juma Abdul (kushoto) usiku huu hoteli ya Double Tree By Hilton

YANGA MAJI YA SHINGO AFRIKA, YAAMBULIA SARE KWA MEDEAMA 1-1


YANGA SC imekamilisha mechi za mzunguko wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika bila ushindi, kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Medeama ya Ghana jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MOURINHO AANZA NA USHINDI WA 2-0 MAN UNITED

Mshambuliaji wa Manchester United, Will Keane (kulia) akishangilia na kiungo Juan Mata baada ya kufunga bao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya

TUME YA VYUO VIKUU(TCU) YATOA UFAFANUZI KUHUSU ALAMA ZA KUDAHILIWA VYUONI


TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016/2017 wanaochukua shahada, huku wanafunzi wengi wakiwa hatarini kukosa nafasi kwa kukosa sifa na vigezo.

Saturday 16 July 2016

WAZIRI MKUU AFUNGUA DUKA LA MSD RUANGWA, KUHUDUMIA HOSPITAL 524

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia hospitali 524 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI AUGUSTINO LYATONGA MREMA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TAIFA YA PAROLE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.