Wednesday 2 March 2016

HALIMA MDEE(KAWE),MWITA WAITARA(UKONGA) WAACHIWA KWA DHAMANA LEO.



Mbunge wa Kawe Halima Mdee na wenzake wanne  wamefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa  shitaka moja la kumjeruhi katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam.


Halima Mdee akiwa na mbunge mwenzie Mwita Waitara wa jimbo la Ukonga  pamoja na makada wengine watatu wa Chadema  wamekana shitaka hilo na wametakiwa kujidhamini wenyewe kwa kiasi cha Shilingi Milioni mbili kila mmoja.

Mahakama hiyo imewaachia kwa dhamana baada ya kuweza kujidhamini



No comments:

Post a Comment