Saturday 30 April 2016

TCRA YATOA ONYO KWA WAFANYABIASHARA WANAOBADILI IMEI ZA SIMU FEKI ILI KUWAHADAA WANANCHI


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa wafanyabiashara wa vifaa vya mawasiliano, kuacha kuwahadaa wananchi kwa kutoa punguzo ili kuwashawishi kununua simu bandia na kutishia kuwafunga miaka 10 jela, faini ya Sh30 milioni au vyote kwa pamoja watakaobainika.

MHANDISI MATHIAS SHOTO ASIMAMISHWA KAZI GEITA


Baraza la madiwani wa halamshauri ya wilaya ya Geita limemsimamisha kazi mhandisi wa halmashauri hiyo  Mathiasi Shoto,kwa  tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi ikiwa ni pamoja na kushindwa kutaja barabara ambazo amekwishakamilisha tangu alipokabidhiwa uongozi huo.

Friday 29 April 2016

MFANYABIASHARA AUAWA NYUMBA YA KULALA WAGENI (GESTI)KWA KUCHOMWA KISU

Mfanyabiashara wa mazao, Eliusta Peter(40),   amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika  nyumba ya kulala wageni wilayani Kilombero.

Thursday 28 April 2016

LUNS HOTEL YANUSURIKA KUUNGUA NA MOTO BAADA YA HITILAFU YA UMEME KUTOKEA KATIKA ENEO LA MITI MIREFU MKOANI GEITA

Hotel ya Luns  iliyopo maeneo ya mtaa wa Miti Mirefu kata ya Kalangalala imenusurika kuungua kwa moto kutokana na hitilafu ya  umeme ambayo ilikuwa imetokea katika nguzo ya mita.

HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA KUBORESHA VITUO VYA AFYA

 
Halmashauri  ya wilaya ya Geita mkoani hapa imedhamiria  kuboresha vituo vya afya ili kuweza kutoa huduma zinazolingana na hospitali ya wilaya ili kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto.

MAJAMBAZI YAUA WAWILI MKOANI GEITA

Watu 2 wameuawa kwa kupigwa  na majambazi waliokuwa  wamevamia katika  baa  inayofahamika kwa  jina la High way pub iliyoko mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala mkoani Geita.

Wednesday 27 April 2016

SERIKALI KUAGIZA NJE SUKARI KIASI

Serikali imesema haitatoa kibali cha kuagiza mchele kutoka nje ya nchi, lakini itaagiza kiasi kidogo cha sukari ili kufidia nakisi iliyopo nchini hivi sasa kwa lengo la kuepusha mfumuko wa bei ya bidhaa hiyo huku ikieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaficha sukari ili kusubiri bei ipande.

WABUNGE MABUBU KUBANWA BUNGENI......NI WALE WANAOSHIRIKI VIKAO VYA BUNGE LAKINI HAWACHANGII CHOCHOTE


Kiti cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio pekee. 

MWANZA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA KWA KUBANA MATUMIZI

Halmashauri ya Jiji la Mwanza, imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 1 baada ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima tangu mwezi Januari mwaka huu na kuzielekeza fedha hizo kwenye utengenezaji madawati 6,840.

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU TAWALA WAPYA WA MIKOA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.

RIPOTI YA CAG YAWAWEKA KIKAANGONI VIGOGO WA BOHARI KUU YA DAWA (MSD)


Ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad imezichanganya Hospitali ya Taifa Muhimbili na Bohari ya Dawa (MSD), huku Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akihitaji maelezo ya kina kuhusu mkanganyiko huo. 

Tuesday 26 April 2016

BREAKING NEWA: RAIS MAGUFULI AIVUNJA BODI YA TCRA NA KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA HIYO DR ALLY YAHAYA SIMBA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua  dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Aprili, 2016

UMOJA WA WAGANGA WA TIBA ASILIA MKOANI GEITA WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA NYANG'WALE



Umoja wa waganga wa tiba asili wilaya ya Nyang’wale mkoani  Geita umempongeza mkuu  wa wilaya mh  Ibrahim Marwa, kwa kutoa ushirikiano ambao umesaidia kupunguza kasi ya mauwaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi.

WAZAZI MKOANI GEITA WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO KUPATIWA CHANJO

Wazazi mkoani Geita wametakiwa kujenga desturi ya kuhakikisha kuwa wanawapeleka kwenye chanjo watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ili kudhibiti magonjwa ya milipuko ambayo yamekuwa yakiwakabili watoto.

Monday 25 April 2016

DENI LA TAIFA LAZIDI KUPAA....LAFIKIA SHILINGI TRILION 33. 5


Deni la Taifa limeongezeka kwa Sh7.05 trilioni, kutoka Sh26.49 trilioni Juni 30, 2014, hadi Sh33.54 trilioni sawa na ongezeko la asilimia 27. 

ASKARI WANNE WANAODAIWA KUMPIGA MVUVI WAANZA KUCHUNGUZWA NA JESHI LA POLISI MKOANI KAGERA.

Askari Polisi wanne kutoka wilaya ya Muleba mkoani Kagera, wanachunguzwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mvuvi mmoja wa kisiwa cha Kunene wilayani Ukerewe Tabibu Kilangi kwa tuhuma za wizi wa injini za mitumbwi zinazodaiwa kupatikana kwa njia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

RIPOTI YA CAG YAANIKA 'MADUDU' KIBAO SERIKALINI


Wakati Rais John Magufuli akipambana dhidi ya ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi na uovu mwingine dhidi ya mali za umma, ripoti mpya ya ukaguzi iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha ana kazi kubwa zaidi kupata ushindi kwenye vita hiyo. 

TAKUKURU YAANZA KUCHUNGUZA MABILIONI YA JAKAYA KIKWETE



Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza fedha za uwezeshaji maarufu kama ‘Mabilioni ya JK’ ambazo hazikurejeshwa na wakopaji nchi nzima.

WANANCHI MKOANI GEITA WATAKIWA KUCHUKUA VIPIMO KABLA YA KUTUMIA DAWA PINDI WANAPOJIHISI KUUMWA

Ikiwa leo ni kilele cha siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa malaria duniani wananchi mkoani Geita wametakiwa  kuacha tabia ya kutumia dawa kabla ya kupata vipimo pindi wanapohisi kuugua na badala yake kufika  katika vituo vya afya ili waweze kupatiwa  tiba sahihi.

WAFANYABIASHARA MKOANI GEITA WALALAMIKIA KUTOZWA USHURU WA JUU

Wafanyabiashara katika soko  linalomilikiwa na chama cha mapinduzi (ccm) kata ya Katoro wilayani na mkoani  Geita wamelalamikia kuwepo kwa gharama kubwa ya utozwaji wa ushuru.

Sunday 24 April 2016

SERIKALI YAHAMASISHA WAWEKEZAJI WA VIWANDA NCHINI

Serikali imewataka wawekezaji wa ndani na nje kutumia fursa zilizopo Tanzania hasa katika eneo la kuongeza thamani ya malighafi mbalimbali.

TANZIA:MWANAMUZIKI NGULI WA CONGO PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA


Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.

Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi


                 Papa Wemba  alipoanguka na kupoteza fahamu katikai ya onesho

Saturday 23 April 2016

WANAWAKE WAWILI WAUWAWA KWA MAPANGA MKOANI GEITA



Wanawake wawili akiwemo mhudumu wa afya wa zahanati ya Kagu iliyopo kijiji cha Kagu Elizabeth Misango [54] na wa pili Helena Paulo [56] mkazi wa kijiji cha Luhuha mkoani Geita wameuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga ikiwemo kuchinjwa shingoni katika matukio mawili na maeneo tofauti usiku wa April 21.

WANANCHI WA KATA YA NYAKUMBU MKOANI GEITA WATAKIWA KUONDOKA MAENEO YANAYODAIWA KUWA NI YA JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM


Wananchi  wa mtaa wa Mwembeni kata ya Nyankumbuku  mkoani Geita wameendelea kusisitiza kuwa hawataondoka katika maeneo ambayo yanasemekana  kuwa ni ya jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi kutokana na kwamba maeneo hayo wana uhalali  wa  kuyamiliki.

WANANCHI WA MJI WA KATORO MKOANI GEITA WAUSHUKURU MGODI WA DHAHABU WA GEITA GEITA(GGM)


Wananchi wa mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, wameendelea kuishukuru kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu (GGM),kwa kutoa msaada wa matibabu kwa waathirika wa midomo sungura.

Friday 22 April 2016

MSHAHARA WA RAIS MAGUFULI WATUA BUNGENI, MBUNGE WA CHADEMA ATAKA UPUNGUZWE NA AKATWE KODI

Suala la mshahara wa Rais, limeibuka tena bungeni ambapo Bunge limeelezwa kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais hawezi kujipunguzia mshahara pindi anapoapishwa kushika wadhifa huo.

SERIKALI KUWEKA MIKAKATI ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KATIKA HOSPITALI YA GEITA


Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa inaboresha huduma za afya katika hospitali ya wilaya ya Geita ikiwa ni pamoja na kuipatia  hadhi ya kuwa hospitali   ya mkoa.

MIUNDOMBINU MIBOVU WILAYANI NYANG`WALE MKOANI GEITA NI KIKWAZO KWA KINA MAMA WAJAWAZITO


Ubovu wa miundombinu ya Barabara na ukosefu wa huduma  za  afya  katika kijiji cha Lubando kilichopo kata ya Shabaka wilayani Nyang`wale mkoani hapa,ni sababu ya akina mama wengi hususani wajawazito kujifungulia njiani  na wagonjwa kupoteza maisha kutokana na kufata zahanati katika kata ya kasamwa.

Thursday 21 April 2016

MTI WAJERUHI WANAFUNZI WAWILI NA KUUA MMOJA WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA


Wanafunzi watatu wakike wa Shule ya Sekondari Msasa iliyoko  Kata ya Runzewe Mashariki wilayani Bukombe mkoani Geita jana wamepondwa na mti wakiwa Shuleni na  kati yao mmoja amefariki dunia na wenzake wawili kujeruhiwa ambapo wamelazwa  katika kituo  cha afya  cha Uyovu mkoani hapa

MAKAMPUNI YANAYOZALISHA BIDHAA NCHINI YATAKIWA KUWEKEA NEMBO BIDHAA ZAO


Serikali kupitia wizara ya viwanda,Biashara na uwekezaji imeyataka makampuni yanayozalisha bidhaa nchini kusajili nembo za bidhaa zao ili kuweza kupata takwimu sahihi ya bidhaa  zizalishwazo  Nchini.

Wednesday 20 April 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WALALAMIKIA KUPANDA KWA BEI SUKARI

Wananchi  mkoani Geita wamelalamikia suala la wafanyabiashara wa sukari kupandisha gharama kutoka katika bei ya shilingi 2000 hadi kufikia shilingi 2500 hali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa wananchi wenye vipato vya chini

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH.MAKONDA ATANGAZA VITA NA WAFANYAKAZI HEWA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

GARI AINA YA HIACE YATELEZA KWENYE KIVUKO NA KUZAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Jeshi la Zimamoto linaendelea kuutafuta mwili wa mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari aina ya Hiace ambalo limetumbukia bahari ya Hindi leo alfajiri mara baada ya kuteleza kutoka kwenye kivuko kilichokuwa kinaelekea upande wa Kigamboni.

Tuesday 19 April 2016

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ATOA UFAFANUZI KWA WANANCHI WAISHIO MGUSU MKOANI GEITA BUNGENI HII LEO



Wananchi waishio  mtaa wa Mgusu wilayani na mkoani Geita wametakiwa  kujua kuwa wanaishi   katika sehemu ya leseni ya utafiti wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita( GGM) na kwamba  eneo hilo bado mgodi haujaona sababu  ya kulichukua.

MKOA WA SHINYANGA WABAINIKA KUWA NA WATUMISHI HEWA 226 KUTOKA 0.

Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.

RAISI JOHN POMBE MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WILSON KABWE



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe kuanzia leo tarehe 19.04.2016.

PICHA:MUONEKANO WA DARAJA LA KIGAMBONI LINALOUNGANISHA KIGAMBONI NA UPANDE WA KURASINI


Daraja la kisasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigamboni na upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. 

Lina barabara sita za magari na moja kwa watembea kwa miguu na pia lina urefu wa mita 680 huku likiwa limegharimu jumla ya shilingi bilion 214.6.

Monday 18 April 2016

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU ASEMA SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMBUA MAJIPU WALA RUSHWA BILA KUJALI HADHI ZAO

Serikali  ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi kwa nguvu zote bila kutetereka.

MKURUGENZI WA WILAYA AMSIMAMISHA KAZI MUUGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI GEITA

toolbox-gloves-np311ws
Kaimu mkurugenzi wa  halmashauri ya wilaya ya Geita Deus  Seif amemsimamisha kazi muuguzi wa hosptali ya rufaa ya mkoa  Fatuma Salumu baada ya kukamatwa akijaribu kutoroka na vifaa tiba vya hosipitalini hapo.

Saturday 16 April 2016

ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU CHACHE MABASI YA MWENDO KASI KUANZA KAZI NCHINI WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA TAASISI HUSIKA


Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mradi wa mabasi yaendayo kasi kuanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA DKT.MWAKYEMBE KATIKA ZIARA YA SIKU MOJA MKOANI GEITA


Serikali imekiri kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa watu katika magereza huku sababu ikielezwa ni ucheleweshwaji wa kesi unaosababishwa na kucheleweshwa  kwa kesi za baadhi ya washitakiwa.

BIBI KIZEE MWENYE UMRI WA MIAKA 84 ABAKWA MKOANI SINGIDA


Pichani ni Bibi kizee mwenye umri wa miaka 84 na mkazi wa Kijiji cha Chungu, tarafa ya Ihanja, wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida akiwa amebebwa na mmoja wa ndugu zake wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Singida kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 (jina lake halikupatikana) anayetuhumiwa kumbaka bibi kizee huyo kwa mara ya tatu sasa ndipo walipofanikiwa kumkamata