Thursday 27 July 2017

MBUNGE WA GEITA VIJIJINI ATOA NENO JUU YA ENEO LA STENDI YA IHANAMILO



Kahimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita akielezea juu ya utatuzi wa tatizo ambalo limeonekana kwenye kijiji hicho juu ya kuuzwa kwa eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwaajili ya matumizi ya stendi.



Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,Joseph Msukuma akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Ihanamilo Kata ya Nkome wakati za zoezi la kuondoa Vigingi ambavyo viliwekwa kwenye eneo ambalo limetengwa kwaajili ya ujenzi wa Stendi ya mabasi kijijini Hapo.



Wananchi wakifuatilia mkutano.

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mh,Joseph Kasheku Msukuma  ambaye pia ni mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita ameongoza mamia ya wananchi wa kijiji cha ihanamilo Kata ya Nkome Wilayani Geita kutoa visiki ambavyo viliwekwa na mtu ambaye inasadikika amenunua eneo la kijiji   linalokadiliwa kuwa ni hekari moja na nusu  ambalo lilitengwa kwa matumizi ya stendi kutoka kwa serikali ya kijiji.

Hatua hiyo imekuja  baada ya Serikali ya Kijiji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ,Bw Thomas Alila na mtendaji wa kijiji Charles Mbilingi kuuza eneo kwa kiasi cha sh ,Milioni sita (6).
Kwa maelezo ya afisa mtendaji wa Kijiji Charles Mbilingi amesema kuwa tarehe 15 mwezi huu walikaa kwenye kikao na wanakijiji na kuamua kwamba wauze eneo hilo  ili liweze kusaidia ujenzi wa shule.

“Tulikaa kama halmashauri ya Kijiji tukajadili namna ya kutatua changamoto ya kukosekana kwa shule kwenye kijiji chetu tulipojadili tukaonelea kwa sababu tuna eneo ni bora tuliuze ili tuweze kupata pesa ambazo zitasaidia ujenzi wa madarasa na hatukufanya peke yetu 
tuliwashirikisha wananchi wa kjiji wakawa wamekubali”Alisema Mtendaji.

Hata Hivyo kutokana na maelezo hayo ya mtendaji wa Kijiji Mbunge  Msukuma amewaeleza wananchi ambao walikuwa kwenye Mkutano wa hadhara kuwa eneo hilo liliuzwa tarehe tano mwezi huu jambo ambalo yeye alilikataa kutokana na faida ambazo zinaweza kupatikana kutokana na uwepo wa eneo hilo.

“Nimesikitishwa sana na kitendo ambacho kimefanyika cha kuuzwa eneo hilo kiasi cha Shilingi milioni sita (6) na mimi nilimpigia simu mtendaji nikamwambia  azirudishe pesa aende halmashauri kuna maelekezo kwa mkurugenzi na tutambue kuna maeneo muhimu lazima yawepo leo(jana)ninakwenda kung’oa visiki vyote”Alisema Msukuma

Katika hali isiyo ya kawaida  Diwani wa Kata ya Nkome Masumbuko Nsembe amejikuta jina lake likiwa limeandikwa kuwa ni miongoni kati ya viongozi ambao walilidhia  kuuzwa kwa eneo  la kijiji.
“Mheshimiwa Mbunge mimi sikuuza nilifika saa kumi na moja nilikuta wakisoma hiyo taarifa ya kuuza lakini mimi niliwaambia kuwa wasiuze eneo hilo kwa hicho kiasi.”Alisema Diwani

Katika hali isiyo ya kawaida wananchi ambao walihudhuria  kikao hicho cha kukubaliana kuuzwa kwa eneo hilo  walipotajwa majina yao walijikuta wakidai kushindwa kujua hali hiyo imetokana na nini na kama waliingizwa mkenge kwenye mauziano hayo.


Kutokana na hatua ambayo mbunge ameifanya ya kuongeza wananchi kutoa visiki wananchi wameshukuru na kusema kuwa walikuwa hawajui  kama eneo lao limeuzwa.

No comments:

Post a Comment