Hali ya Afya ya Spika
mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa
matibabu zaidi.
Habari za
uhakika zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya
afya yake kubadilika ghafla.
“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa
nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu
amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.
“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa
kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai wake…hii tabia
ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.
“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu
natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake
siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.
Septemba 19, mwaka
huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda
sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.
Siku iliyofuata Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.
Sitta ameshika
nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010,
uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.
No comments:
Post a Comment