Leo September 20 2016 taarifa
iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.
Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza
tarehe 05 Septemba, 2016. Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda
wake.
Wakati huo huo, Rais
Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba,
2016. Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali
ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi
Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba,
2016. Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali
ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus
Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016. Balozi
Ladislaus Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Christopher
Celestine Liundi ambaye amemaliza muda wake.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti,
2016 Fidelis Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
wa LAPF.
No comments:
Post a Comment