Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa Mkutano
wa Kumi na Nne wa Bodi ya Wahandisi nchini leo JIjini Dar es Salaam.
Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka wahandisi nchini kufanya
kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia
ujezi na uendelezaji viwanda.
Amesema hayo leo
jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na
kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili
kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.
“Mkiamua nchi iende kwenye uchumi
wa kati inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi
uzalendo unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema
Rais Magufuli.
Aidha amewataka
kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye
utendaji kazi na miradi ya maendeleo.
“Tumemsikia waziri akisema
serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni
mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi
kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli
Akimkaribisha rais
Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof
Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya
ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele
ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.
“serikali inafanya
jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu
moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika
kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais
kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika miradi mikubwa ili
kujifunza kupitia miradi hiyo.
Aidha Mhandisi
Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100
kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari
nchini.
akizungumza katika
mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe
mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.
Katika kuhakikisha
miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku
ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema
Makonda
No comments:
Post a Comment