Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali wakibadilisha mawazo juu ya mradi huo ambao umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)
Hapa ndio tank kubwa la mradi wa maji unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania na
umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa
Amina Masenza amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Rural Development
Organization (RDO) Tanzania kwa kufanikisha kupatikana kwa maji katika baadhi
ya vijiji vya wilaya ya Kilolo na Mufindi ambayo itakuwa njia moja wapo ya kuchochea
maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa
kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nandala’ Masenza alisema kuwa
amefurahishwa na mfumo ambao unatumiwa na shirika hilo kwa kutoa huduma ya maji
kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.
“Mradi wowote ule ukiwa na
ushirikiano mkubwa na wananchi mara nyingi wananchi wanautunza mradi huo kwa
kuudhamini na kuulinda,hivyo nawapongeza RDO kwa kufanya maamuzi sahihi ya
kubuni mradi huo pamoja na wananchi” alisema Masenza
Masenza alisema kuwa mradi
huo wa maji utatoa huduma kwa wananchi wengi na taasisi binafsi nyingi hivyo
wananchi wanatakiwa kuutunza na kuudhamini ili udumu kwa muda mrefu na kuondoa
tatizo la maji ambalo limekuwa kero ya muda mrefu.
Nimesikia kwenye
risala yenu kuwa mradi huu utahudumia kata zifuatazo
Ifwagi,Mdabulo,Ihanu,Luhunga,Mtitu na Kising’a na vijiji vitakavyopata huduma
hiyo ni
Igonongo,Ludilo,Kidete,Ikanga,Nandala,Ibwanzi,Isipii,Mkonge,Lulanzi,Luhindo,Barabara
mbili na Isele hivyo ukiangala utagundua kuwa mradi huu ni mkubwa na upaswi
kupuuzwa kwa maendeleo kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo umepita.
“Jamani wananchi ambao
mmepata bahati ya kupitiwa na mradio huu mkubwa wa maji mnapaswa kuulinda na
kuudhamini kwa kuwa ni mmoja ya mradi mkubwa ambao unapunguza adha ya
upatikanaji wa maji ambayo hapo awali ilikuwa kero kubwa” alisema Masenza
Kwa upande mkurugenzi
mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization
(RDO) Tanzania Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umegharibukiasi cha
shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)
ambao ndani yake kuna pesa zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kusaidia
kupata huduma ya maji.
“Sisi kama RDO ambao
ndio wafadhili namba moja wa mradio huu wa maji tumechangia kiasi cha shilingi
milioni themenini na sita,laki nane ishirini na moja elfu (86,821,000) na
wananchi walichanga kiasi cha shilingi milioni nane,laki sita themenini na
mbili na mia moja (8,682,100)” alisema Filipatali
Filipatali
alisema kuwa mradi huo wa maji utazaliza ujazo wa lita 776
kwa vijiji vyote ambazo vinatumia huduma hiyo ya maji na pia wananchi
watakao pata huduma hiyo ni 10,874 kwa vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo
na jumla ya taasisi 18 nazo zitanufaika na huduma hiyo.
“Mkuu wa mkoa sasa
ukiangalia kwa ujumla ndio utagundua kuwa ni mradi ambao utakuwa unakomba
wananchi wengi waliokuwa wanapata tabu juu ya kupata maji hivyo naomba pia
nisisitize wananchi kuutunza na kuchangia kwa malipo kidogo kwa ajili ya
ukarabati wa mashine na mitambo mingie inayosukuma maji hayo ili isihalibike” alisema Filipatali
Filipatali alisema
kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto zifuatazo baadhi ya watumiaji maji
kutochangia, viongozi kutotimiza majukumu yao kama kutohudhuria mikutano ya
mapato na matumizi,watumiaji maji kutotilia mkazo elimu wanayopewa na wataalamu
wa maji,siasa kuingia mfumo mzima wa mradi huu na baadhi ya serikali za vijiji
kuchukulia mapato ya miradi ya maji kama sehemu ya mapato ya serikali
kitu ambacho sio kweli mfano kjiji cha Lidilo
“Hizi changamoto
zimekuwa kero sana kwenye miradi ambayo imekuwa inatekelezwa kwenye maeneo
husika hivyo niwaombe viongozi wa kiasa wawe wa kwanza kutoa elimu juu ya
miradi ambayo inafaida na kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao” Filipatali
No comments:
Post a Comment