Thursday 8 September 2016

MKUU WA WILAYA YA GEITA AAGIZA KUHAMISHWA KWA MTENDAJI WA KIJIJI CHA BUJURA















Mkuu  wa  wilaya ya Geita Herman Kapufi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuhakikisha  anamuhamisha Mtendaji  wa Kijiji cha Bujura Sekile Mhagwa  kuanzia  jana  kutokana na  kuwa na tuhuma za kutumia fedha kiasi cha Sh.Millioni 9 kinyume  na matumizi ya fedha hizo,
Miongoni mwa fedha hizo kulikuwa na fedha za watoto waishio katika  mazingira magumu na zingine za watu ambao wameathirika  na Virusi  vya Ukimwi  (VVU) na pesa nyingine ya mfuko wa Jimbo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya kufanya Ziara yake ya Kikazi yenye lengo  la kuzungumza na Wananchi  na  kutatua changamoto  ambazo zimekuwa zikiwakumba Wananchi  wa Wilaya ya Geita katika mkutano na Wananchi Kata ya Bujura

Diwani wa Kata hiyo Amina Kanijo  amefikisha malalamiko yake mbele ya Mkuu  wa Wilaya akimtuhumu mtendaji wa Kata kutumia Fedha kinyume na utaratibu uliokuwa umewekwa.
Na kutokana na malalamiko hayo ilimlazimu  Mkuu wa wilaya ya geita kutoa maagizo ya kuhakikisha mwalimu ambae ametuhumiwa na matumizi ya fedha kukamatwa lakini pia  na  mtendaji  hata kama amelipa fedha hafai kuendelea kubaki katika kituo hicho cha kazi hivyo amemuagiza Mkurugenzi kumpatia uhamisho wa kwenda   kufanyia   kazi mahali   pengine.


Pia Herman Kapufi aliwaagiza Watumishi wote  kuhakikisha wanakuwa na maadili katika kuwatumikia Wananchi na kuachana  naTtabia ya kuwa kero katika  jamii wanazoziongoza.

No comments:

Post a Comment