Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewapongeza Wachezaji wa
Kilimanjaro Queens kwa niaba ya serikali na kwa niaba ya watanzania kwa kazi
nzuri waliyoifanya mpaka kuwa mabingwa wa kwanza wa Kombe la CECAFA kwa mpira
wa miguu kwa wanawake Afrika Mashariki na Kati.
Pongezi hizo
zimetolewa na Waziri Nnauye alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini
Dar es Salaam.
“Kama serikali ni
vyema kuipongeza timu yetu ya Kilimanjaro Queens kwa kuiwakilisha vizuri
Tanzania katika michuano CECAFA na kuibuka mabingwa kwa kuweza kuruka vizingiti
vyote vilivyokuwepo katika muchuano hiyo” alisema Mhe. Nnauye
Serikali itaendelea
kuweka nguvu ya kutosha na kuungana na timu zetu kuwasaidia kuhakikisha
wanafanya vizuri zaidi katika michezo mbalimbali, amesema Mhe. Nnauye.
Mhe. Nnauye amesema
kuwa Tanzania inaanza kuona matunda ya uwekezaji wa muda mrefu kwani haikuwa
kazi raisi kwa Kilimanjaro Queens kufikia fainali na kuwa mabingwa kwa
kupambana na timu ngumu na kuweza kushinda.
Aidha Mhe. Nnauye
amewahaidi wachezaji wa Kirimanjaro Queens kuwaalika bungeni katika Bunge
lijalo kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaandalia mechi ya kirafiki kutambua
mchango wao wa kuipeperusha bendera ya Tanzania kati yao na wabunge wanawake.
Timu zilizoshiriki
katika michuano ya kombe la chalenji la CECAFA ni pamoja na Tanzania, Burundi,
Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na mwenyeji Uganda. Mashindano ya
Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za wanawake yamefanyika kwa mara ya kwanza
jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa
ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment