Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akikata utepe ishara ya uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Maguguli Leo
9 Machi 2018 amezindua jengo jipya la Benki ya CRDB Tawi la Chato Mkoani Geita.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe Dkt. Magufuli amesema kuwa uwepo wa
Benki hiyo utarahisisha huduma za uhifadhi fedha kwa wafanyabiashara wa samaki
Wilayani Chato sambamba na wananchi ambao kwa kiasi kikubwa katika msimu wa
Kilimo wamenilima Pamba kwa wingi.
Ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuzifungia baadhi ya Benki
nchini na kuzipa onyo zingine ambazo zilikuwa zinafanya kazi kwa mazoea na
kwenda kinyume na utaratibu wa sheria za uendeshaji.
Alisema ni bora kuwa na Benki chache nchini ambazo zinaweza kuwahudumia
wananchi wengi hususani masikini kama ilivyo CRDB ambayo imewafikia kwa kiasi
kikubwa wananchi vijijini hivyo kuendelea kuzifungia Benki zote ambazo
zimeshindwa kuendesha vyema shughuli zake na kusalia kufanya huduma Jijini Dar
es salaam pekee.
Rais Magufuli ameiomba benki ya CRDB kupunguza riba ya mikopo kwani ni
asilimia 16 pekee ya watanzania ndio wanaohudumiwa kwenye Benki nchini hivyo
ili wananchi wote waweze kukopa na kuweka mitaji yao midogo kwa ajili ya faida
yao ya Sasa na badae ni lazima kuwa na riba rafiki kwa wananchi.
JPM ameipongeza Benki hiyo kwa kuajiri wafanyakazi wapatao 3200 tangu
ilipoanza rasmi nchini mwaka 1972 wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya
kwanza chini ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeielewa dhana
halisi ya kuwasaidia wananchi vijijini kutokana na usumbufu mkubwa wanaoupata
katika huduma za kifedha.
Alisema kuwa anayo imani kubwa na Benki ya CRDB kwani naye ni mteja wa
benki hiyo hivyo ili kuendeleza mahusiano mema tayari seikali imelipa Deni lote
la shilingi Bilioni 16 ambalo ilikuwa inadaiwa na benki hiyo kutokana na mikopo
katika miaka ya nyuma.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewahamasisha wananchi kutunza fedha
zao benki na kuachana na dhana ya kuhifadhi fedha majumbani jambo ambalo
ni hatari kwa usalama wa fedha hizo na maisha yao wenyewe.
Mhe Magufuli amesisitiza watanzania kuwa wazalendo huku akisema kuwa
anatambua kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wamesalia na jukumu la kuandika
katika mitandao na vyombo vya habari mambo ambayo ni kinyume na utendaji wa
serikali jambo ambalo ni uchonganishi dhidi ya wananchi na serikali yao.
Aidha, Mhe Rais Magufuli alikataa ombi la Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei aliyetaka Benki hiyo kuitwa CRDB JOHN
POMBE MAGUFULI-CHATO huku akisema kuwa isalie kuitwa CRDB tawi ka CHATO.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania, Dkt
Charles Kimei ametoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kukubali kuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Benki hiyo huku akielezea namna ambavyo amekuwa na dhamira
ya dhati ya kuwainua watanzania kupitia rasilimali zao jambo ambalo litawanufaisha
na kuwainua kiuchumi.
Alisema kuwa Benki hiyo itaendelea kubuni njia nzuri za mikopo huku
akisisitiza kuwa Benki hiyo kuendelea kuwasaidia wananchi kupitia SACCOS zao
kupata mikopo nafuu ili kujinufaisha kwa kuwa na uchumi imara utakaowawezesha
kukuza biashara zao.
Sambamba na hayo pia amekubali ombi la Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe
Medard Kalemani ambaye ni Waziri wa Nishati la kujenga uwanja wa kisasa wa
Mpira wa miguu ambapo kwa niaba ya Benki hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini
Benki ya CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari amekabidhi Hundi la Shilingi
Milioni 50 kwa ajili ya hatua za mwanzo za kuanza ujenzi wa uwanja huo huku
akiahidi Benki hiyo kuwa wadhamini wa timu ya mpira wa miguu ya wilaya ya
Chato.
Dhifa ya uzinduzi wa Benki hiyo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali
akiwemo Waziri Wa Nishati Mhe Medard M.Kalemani (Mb), Naibu Waziri wa
Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb), Mkuu Wa Mkoa Wa Geita Mhandisi Robert
Gabriel, Naibu Waziri Wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijazi (Mb), Naibu Gavana
Wa Benki Kuu Tanzania Dkt Bernard Yohana
Kibese, Balozi Wa Denmark nchini Tanzania Mhe Einar Hebogard
Jensen, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari,
Mkurugenzi Mtendaji CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei, na Wabunge wa majimbo
mbalimbali ikiwemo jimbo la Busanda na Mbogwe.
No comments:
Post a Comment