Wananchi mkoani Geita wameiomba Serikali kuanza
kuwapatia Mabaki ya Mawe Maarufu Magwangala kama ilivyo elekezwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati wa Ziara yake mkoani hapa.
Rais Magufuli alifanya Ziara yake mnamo julai 30 mwaka huu mkoani hapa na
kukutana na kilio cha Wananchi
wanaodai kuwekewa zuio la kutumia mawe
yenye mabaki ya dhahabu (magwangala) kwa lengo la kusaga na kuchenjua ili
kupata dhahabu, ndipo akatoa muda wa
wiki tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na baraza la
taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) kufanya tathimini na
kuwaruhusu Wachimbaji wadogo kutumia Magwangala.
Wakizungumza kwa
Nyakati tofauti baadhi ya wananchi mkoani hapa wamesema kuwa tangu Rais
Magufuli atoe kauli hiyo ni takribani
mwezi mmoja umekwisha kupita lakini bado hawajaanza kupewa Magwangala
hayo hali ambayo imekuwa ikiwapa wasiwasi na kushindwa kujua ni lini hatima hiyo
itakamilika.
Hata hivyo mmoja kati ya Viongozi wa baadhi ya vikundi vilivyoundwa
kwa ajili ya kupatiwa Magwangala ambaye yeye ni Katibu wa kikundi kimoja hapa
mjini kinachofahamika kwa jina la Majiko group chenye makazi yake Mtaa wa Msalala road uliopo wilayani na mkoani hapa Bw.Elia Elinathani ambapo amesema kuwa amekuwa
akilifuatilia mara kwa mara jambo hilo.
Suala hili Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi
ametoa ufafanuzi juu ya hayo madai
wakati alipokuwa katika moja kati ya ziara zake za kikazi katika kata ya Bujura
mkoani Hapa.
No comments:
Post a Comment