Leo September 14 2016 Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt.
Ramadhani Kitwana Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dkt. Ramadhan Kitwana Dau alikuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Balozi Dkt.
Ramadhani Kitwana Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa
Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wakati huo huo, Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu
aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita. Walioapishwa ni kwanza,
Eliya Mtinangi Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa kwanza wa Mkoa wa Songwe
ulioanzishwa rasmi Mwezi Februari 2016.
Pili, Adoh Stephen Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mara. Adoh Stephen Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict
Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.
Tatu, Tixon Tuliangine Nzunda
anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Tixon Tuliangine Nzunda
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies Emmanuel Pangisa ambaye
amestaafu. Baada ya kuapishwa, Balozi Ramadhani Kitwana Dau na Makatibu
Tawala wote watatu wamekula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma
kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na
kushuhudiwa na Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment