Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiongea na wajumbe wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) wakati akiizindua leo Jijini Dar es
Salaam, ambapo ameitaka bodi hiyo kushika miradi mikubwa ya uwekezaji na
kuhakikisha inairudisha katika hali yake ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa
kati kupitia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda.
Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage amesema Shirika la Taifa Maendeleo ya Viwanda (NDC) ndio injini ya
kushikiria sekta ya viwanda na hivyo inatakiwa kuhakikisha ndani ya miaka minne
inakuwa viwanda hata vitatu katika kuweza kufikia uchumi wa kati.
Mwijage ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa BAodi
mpya ya Wakurugenzi NDC, amesema kuwa bodi lazima ifanye kazi kuhakikisha
inashikiria viwanda vikubwa ambayo vitafanya taifa kuwa na maendeleo ya
kiuchumi kutokana miradi iliyopo chini ya NDC.
Amesema kuwa mradi wa kwanza ni ule wa Liganga na
Mchuchuma unatakiwa kufutika midomoni mwa watu kwa kuanza kuzalisha
kutokana na muda mrefu umekuwa ukizungumzwa.
Mwijage amesema kuwa kutokana bodi hiyo
kuwa na watu wa kila sekta muhimu hivyo wanahitaji kukutana mara kwa mara hata
bila kulipwa posho ili mambo yeande na kuleta tija kwa taifa.
Amesema kuwa miradi mikubwa ikikamilika nchi itakuwa
imepiga hatua kimaendeleo na kuweza kufikia uchumi wa kati wa
viwanda vyenye kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa bodi wa NDC, Dk, Samwel
Nyantahe amesema kuwa watafanya kazi kwa karibu na wizara ikiwa ni pamoja na
kutembelea miradi yote na kuweza kuanza kufanya kazi kwa nguvu.
Amesema Rais Dk. John Magufuli amemuamini hivyo
watatimiza wajibu kwa kushirikiana na bodi hiyo katika sekta ya viwanda.
No comments:
Post a Comment