Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe
Robert Mugabe
Ameambia Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji
uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi
zinazokabili taifa hilo.
“Ni wazi kwamba umri wake na hali
ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza
kulinusuru taifa hilo,”.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa
hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi
huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe
umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana
ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.
Khama anasema kuwa ataondoka
afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu
viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu.
No comments:
Post a Comment