Baraza Kuu la Uongozi
la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa lililokutana Zanzibar leo limemfukuza
uanachama Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba.
Taarifa kutoka katika mkutano chama hicho unaeleza kuwa, wajumbe wote
waliohudhuria wamepiga kura ya kuridhia kufukuzwa uanachama kwa Prof. Lipumba.
Hatua hii imekuja
ikiwa ni siku chache tangu Prof. Lipumba kurejea na kusema kuwa yeye ni
mwenyekiti halali wa chama hicho kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Msajili wa
Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi.
Baraza Kuu la Uongozi
la Taifa la CUF limefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10
(1)(c).
No comments:
Post a Comment