Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiongea na wajumbe wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) wakati akiizindua leo Jijini Dar es
Salaam, ambapo ameitaka bodi hiyo kushika miradi mikubwa ya uwekezaji na
kuhakikisha inairudisha katika hali yake ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa
kati kupitia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda
Wajumbe
wa Bodi ya wakurugenzi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Mhe. Charles Mwigaje, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda
,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Shirika la Taifa Maendeleo ya Viwanda (NDC) ndio injini
ya inayoendesha sekta ya viwanda na hivyo inatakiwa kuhakikisha ndani ya miaka
minne inakuwa viwanda hata vitatu katika
kuweza kufikia uchumi wa kati.
Mwijage ameyasema
hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi ya shirika hilo,ambapo
ameitaka bodi kufanya kazi ili kuhakikisha inashikilia viwanda vikubwa ambayo
vitafanya taifa kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Amesema kuwa kazi
ya bodi hiyo kwa kuaznia ni kuangalia miradi na viwanda ambavyo kwa sasa
havifanyi vizuri ikiwamo mradi wa Liganga na Mchuchuma, kiwanda cha matairi cha
general tyre kilichopo Arusha na vingine ili na dhumuni ni kuhakikisha vinaanza
kuzalisha.
Mwijage amesema
kuwa kutokana bodi hiyo kuwa na watu wa
kila sekta muhimu hivyo wanahitaji kukutana mara kwa mara hata bila kulipwa
posho ili mambo yeande na kuleta tija kwa taifa.
Amesema kuwa
miradi mikubwa ikikamilika nchi itakuwa imepiga hatua kimaendeleo na kuweza
kufikia uchumi wa kati wa viwanda vyenye
manufaa kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa
bodi wa NDC, Dk, Samwel Nyantahe amesema
kuwa watafanya kazi kwa karibu na Wizara ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi
yote na kuweza kuanza kufanya kazi kwa nguvu.
Amesema Rais Dk.
John Magufuli amemuamini hivyo watatimiza wajibu kwa kushirikiana na bodi hiyo
katika sekta ya viwanda.
No comments:
Post a Comment