Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza leo Jijini
Dar es Salaam na wachezaji wa Serengeti Boys katika hafla fupi ya kuwakabidhi
Shilingi Milioni Tano kama motisha kabla ya mechi ya leo dhidi ya
Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Bw. Jamali Malinzi
akitoa maelezo juu ya maaandalizi ya mechi kati ya Serengeti Boys na
Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Kocha wa Serengeti Boys Bw. Bw.Bakari Shime akimshukuru
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo
Pichani) kwa kuwapa motisha wachezaji kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na
Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame akiahidi kwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani)
kuibuka na ushindi dhidi ya Congo-Brazaville katika mechi itakayofanyika katika
Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akimkabidhi Millioni tano Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame kama
motisha kabla ya kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika
katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Baadhi ya wachezaji wa
Serengeti Boys wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika hafla fupi kabla ya mechi yao dhidi
ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa kiasi cha shilingi
million tano kwa timu ya Serengeti Boys kama motisha katika mchezo wao dhidi ya
Congo Brazivile utakayochezwa leo katika Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es Salaam.
Akikabidhi pesa hizo
leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Waziri Nape amewataka wachezaji hao kujituma
zaidi katika mechi hiyo ili wapate ushindi utakaowawezesha kufuzu katika
fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 .
“Watanzania wote tupo pamoja
na nyie endeleeni kujituma kama mlivyofanya katika hatua ya kwanza na ya
pili, Sisi kama Serikali tunawaunga mkono na tunawatakia
heri ili mlete heshima kwa Taifa.”Alisema Mhe. Nape.
Kwa upande wa Kocha wa
Timu hiyo Bw.Bakari Shime amemuhakikishia Waziri na Watanzania kwa
ujumla kuwa mechi ya leo watahakikisha wanapata ushindi kwani wamejiandaa
vizuri na wachezaji wote wapo tayari kuivaa Congo Brazavile.
Aidha Nahodha wa Timu hiyo
Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi
kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata maagizo
kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata
ushindi.
“Tunashukuru sana kwa
motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate
ushindi ili tusonge mbele zaidi ” Aliongeza Nahodha Makame.
Timu hiyo
ya vijana chini ya umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys)
inashiriki kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana
yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment