naibu waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni azindua wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani, Kitaifa Mjini Geita leo
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini Mohamed Mpinga akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani.
Washiriki wa maonyesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika
maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mjini Geita leo.
Maadhimisho
ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani
yamezinduliwa Rasmi leo Mkoani Geita katika viwanja vya Kalangalala na Naibu Waziri wa mambo ndani Mh.Ahamed Masauni,
huku ajali za waendesha piki piki maarufu boda boda zikiendelea kushika kasi kubwa zaidi nchini.
Akitoa taarifa ya jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani, Kamanda wa kikosi cha
usalama Barabarani Nchini Mohamed Mpinga amesema kuwa Baraza la taifa la usalama barabarani
nchini limekuwa na mikakati mbali mbali
ya kukabiliana na ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza hususani ni zile
ambazo zinachangaiwa na uzembe
barabarani.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Edwin Ngonyani ambaye ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani
nchini, amefafanua kuwa pamoja na jitihada ambazo zinafanywa na Serikali bado
kuna tatizo kubwa la Madereva na wapanda pikipiki kutokujali Sheria na kanuni za usalama barabarani.
Aidha mgeni rasimi katika maadhimisho hayo Mh.Ahamed masauni amemtaka kila mtumiaji wa barabara
kupambana kwa nguvu na mali katika
kutokomeza ajali za barabarani na kwamba
wajibu huu sio wa serikali tu bali
wananchi nao wanahusika huku akitaja idadi ya ajali zilizotokea kwa mwaka huu.
Mkuu wa mkoa wa geita Meja Jenerali Mstafu ezekiel Kyunga
ametoa Shukrani kwa Baraza la Usalama Barabarani kufanyia maadhimisho ya wiki ya nedna kwa
usalama barabarani mkoani geita akiamini kuwa ni moja kati ya njia ya kutangaza
Mkoa wa Geita.
No comments:
Post a Comment