Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu
nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za
kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu
ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya
watu 16 ,mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.
Kufuatia
kuahirisha ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha katika sherehe hizo za kuapishwa
kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu
Rais Mteule wa
Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika
keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.
Imetolewa na,
Jaffar
Haniu
Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar Es
Salaam
11
Septemba, 2016
No comments:
Post a Comment