Waandamanaji nchini Congo DRC
Watu wengine kadhaa wameuawa katika siku
ya pili ya machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana, huku makao
makuu ya vyama vitatu vya upinzani yakichomwa moto.
Hayo yamejiri katika wimbi jipya la makabiliano kati ya
polisi na wapinzani wa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila
Machafuko yalizuka upya baada ya
Jumatatu ya umwagaji damu ambapo makundi ya upinzani yamesema zaidi ya watu 50
walikufa katika maandamano ya kudai Rais Kabila ajiuzulu.
Katibu wa chama kikuu cha
upinzani cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), Felix Tshisekedi
amelilaumu kundi la makomando la utawala kwa kuyachoma makao makuu ya upinzani.
Maiti mbili zilizoungua
zimeonekana katika afisi za chama hicho.
Waandishi wa habari wa shirika la
habari la Ufaransa, AFP wamesema watu wengine wawili wamechomwa wakiwa hai na
mwingine mmoja kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment