Kutokana na Madhara ambayo yamejitokeza katika Kijiji
na Kata ya Busanda kusambaa kwa
Sumu ya Sayanaidi, Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) imeguswa na tukio hilo na
imetuma wataalam kwa ajili ya
kutatua tatizo ambalo wananchi wameendelea kuathirika kutokana
na baadhi yao kulamba na kunusa
Sumu hiyo.
Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi huo Bw.Manase
Ndoroma amesema kuwa wao kama Mgodi wamesikia
Janga hilo na kwasababu wao wana uwezo
wa kutatua
Janga hilo ndio maana wameguswa na kuamua kutoa msaada kwa watu
ambao wamekwisha athirika na baada ya kusikia kwamba kuna kifo cha mtoto wa miaka minne ambaye alilamba sumu
hiyo na kupoteza maisha.
Baadhi ya Wananchi ambao wamedhurika na Sumu hiyo
Bi.Maria Kaziza na Bw.Kaverwa Lubuga, wamesema
kuwa wameathirika kutokana na kwamba
mifugo mingi imepoteza maisha pamoja na wao kwa sasa hali za afya wanajisikia sio nzuri kwani makoo
yamekuwa yakikauka kutokana na kutumia Sumu hiyo.
Hata hivyo Diwani wa kata hiyo Elias Kisome amelaani kitendo
cha wamiliki wa machimbo madogo kusafirisha Sumu kwa
njia ya Pikipiki na badala yake
kutumia vyombo ambavyo ni vya
uhakika vya kusafirishia Sumu.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mponjoli Mwabulambo amesema yuko nje ya Mkoa na Habari hizo
amezisikia na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha Sumu
hiyo.
No comments:
Post a Comment