Waziri Mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na masuala ya uchumi katika
kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka
kujua hali ya uchumi ilivyo kwa sasa hapa nchini.
Waziri Mkuu
amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha
uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa kushirikiana na taasisi
za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati kama ilivyoanishwa kwenye ilani ya
uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi
Akizungumza kuhusu suala la midororo wa upokeaji wa
mizigo katika bandari nchini, Waziri Mkuu amesema kuwa mdororo huo umetokana na
kupungua kwa kiasi cha mizigo na kushuka
kwa uchumi duniani.
Katika suala ya mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na
Vikindu, Waziri Mkuu amesema kuwa usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku
serikali ikiahidi kupambana vitendo vya mauaji kwa raia na askari katika maeneo
mbali mbali nchini.
“Serikali imesikitika sana na jambo hili la mauaji
hivyo itahakikisha wauaji hao wanawekwa katika mikono ya Sheria na kuongeza
ulinzi kwa maeneo yote nchini kwa kuanzia ngazi ya vitongoji” alifafanua Waziri
Mkuu.
Mbali na hayo Waziri Majaliwa ametoa wito kwa
wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuthibiti matukio hayo.
Kuhusu suala la uwepo wa tozo katika zao la korosho swali
limeibuliwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa
amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya
kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika zao la korosho.
No comments:
Post a Comment