Utoaji wa Tuzo hiyo ya uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba na hafla ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Speak up Afrika. Hafla hiyo iliyofanyika jana Alhamisi Jijini New York ilikuwa pia ni sehemu ya kuhamasisha uchangiaji wa shughuli za Taasisi hiyo.
Mchango ambao
umetambuliwa na Speak Up Afrika, taasisi ambayo imekuwa
ikifanya kazi kwa Karibu na Rais Mstaafu Kikwete, ni katika maeneo
ya upelekaji na usambazaji wa huduma za msingi za afya hususani afya ya
mama na mtoto, udhibiti wa ugonjwa wa malaria kupitia
kampeni ya malaria haikubaliki ,usambazaji wa vyandarua vyenye
viatilifu, kampeni ya lishe bora, na kampeni ya chanjo
kwa watoto.
Pamoja na
kutambua juhudi za Rais Mstaafu Kikwete katika
kuyasemea maeneo hayo, Taasisi hiyo kupitia Mkurugenzi wake
Mtendaji Bi. Kate Campana pia imemtambua kama kiongozi
ambaye amekuwa mstari wa mbele wa kulisema Bara la
Afrika kila mara alipopata fursa ya kufanya hivyo
wakati akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu.
Rais kikwete ameelezwa
katika hafla hiyo iliyowashirikisha wadau wa kada mbalimbali, kama
kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu wengi kujitolea kwaajili ya
watu wenye mahitajio ya kupata huduma za msingi za kijamii ambazo au
wameshindwa kuzipata kutokana na kipato kidogo au haziwafikii kabisa.
Akipokea Tuzo
hiyo, Rais Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo ni ya watoto wote
waafrika ambao ndio waliomfanya asimame mbele ya wageni
waalikwa.
“ Ni kwa sababu yenu
ndio sababu nimetenga muda wangu baada ya kustaafu kusukuma mbele agenda
ya kuboresha maisha yanu. Ninafanya hivyo kwasababu makuzi yangu yalikuwa
kama ya mtoto yeyote yule wa kiafrika, nimeyaishi maisha
wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa fika hamu na kiu yao ya kuwa na
maisha bora na afya njema”. Akasema Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Akaongeza kuwa
, mafaniko ambayo ameyapata katika juhudi hizo za kufikisha
huduma za msingi za kijamii kwa makundi yenye mahitaji
yametokana na mambo mawili makubwa moja ni aina ya uongozi
alioutumia kusukuma harakati hizo. Na pili uhamasishaji uliofanyika
katika kupiga vita malaria kupitia Speak Up Afrika na
kampeni yao ya malaria haikubaliki.
“ Nisingeweza
kuyafanya niliyoyafanya bila uungugwaji mkono na
ushirikiano wa karibu nilioupata na ninaoupata kutoka taasisi za
kimataifa ikiwamo hii ya Speak Up Afrika. Ndio maana
kwa mfano, tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa theluthi
mbilli, tumefanikisha upatikanaji wa chanjo kwa asilimia 96 kwa
watoto wote na kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kwa
nusu.” Akaeleza Kikwete na kushangiliwa tena.
Akasema, anamini
katika ushirikiano na wadau mbalimbali kama akina Ray Chambers kupitia
kampeni ya hakuna tena malaria, Taasisi ya Bili na Melinda Gates na
Gavi Vaccination Alliance ambayo anashirikiano nayo kwa
karibu katika kampeni ya chanjo kwa wote.
Rais Mstaafu
amewahakikishia watendaji wa Speak Up Afrika kwamba
ataendelea kufanya kazi nao kwa karibu kutokana kile alichosema
amejionea mwenye kazi nzuri wanayoifana.
Akawasihi
wadau mbalimbali kuichangia taasisi hiyo kwa kile alichosema,
inafanya kazi kubwa ya siyo tu kufikisha huduma za kijamii pale
zinapotakiwa lakini pia imekuwa ni kipaza sauti cha Afrika.
Wengine waliopewa Tuzo
kwa kutambua michango yao kwa jamii ni pamoja na Professa Awa
Marie Coll- Seck, Waziri wa Afya wa Senegal, Bibi Toyin
Saraki, mwanzilishi wa Taasisi ya Wellbeing Afrika
ambayo pia imekuwa ikitoa elimu na misaada kwa wanawake na watoto
pamoja na elimu kwa wakunga na kutambua kazi nzuri, kubwa na ngumu
ya kuwahudumia wanawake wenzao wanapojifungua. Na Bwana Kabirou
Mbodje ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Wari.
Taasisi ya
Speak Up Afrika imeanzishwa na wanawake na inaongozwa
na wanawake. Ni taasisi ambayo imejijengea uweo na sifa kubwa ndani ya
kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.
No comments:
Post a Comment