Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akiwasili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi kati ya
Serengeti Boys na Congo Brazaville ambapo Serengetri iliibuka na ushindi wa
Goli 3 kwa 2.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akishanglia pamoja na mashabiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza katika mechi kati ya Serengeti
Boys na Congo Brazaville ambapo Serengetri iliibuka na ushindi wa Goli 3 kwa 2.
Mshambuliaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Nkomolo akishangilia mara
baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Congo Brazaville katika Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Slaam Serengeti ilishinda kwa jumla ya goli 3 kwa 2.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na waandishi wa habari Jijini
Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville
iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016 Serengeti ilishinda kwa
jumla ya goli 3 kwa 2.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akiwapongeza wachezaji wa Serengeti Boys Jijini Dar es Salaam mara baada
ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika
katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016 Serengeti ilishinda kwa jumla ya goli 3
kwa 2.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Serengeti Boys wakiwashukuru mashabiki mara baada ya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na Congo Brazaville ambapo Serengeti Boys iliibuka na ushindi wa goli 3 kwa 2.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa kiasi
cha shilingi Millioni moja kwa kila goli litakalofungwa na Serengeti Boys
katika mechi ya marudiano nchini Congo Brazaville.
Ametoa ahadi hiyo
wakati akiongea na kuwapongeza wachezaji hao mara baada ya kumalizika kwa
mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 17 kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Congo Brazaville uliofanyika
katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
“Kwa niaba ya
Watanzania wote nawapongeza kwa mchezo mzuri mliouonesha na kuibuka na ushindi
lakini bado mnatakiwa kujituma kama mlivyofanya katika mechi hii na naahidi
kutekeleza ile ahadi yangu ya laki tano kwa kila goli na nitatoa tena kwenu
Millioni moja kwa kila goli mtakalofunga Congo Brazaville.”Alisema Mhe. Waziri
Nape.
Kwa upande wa Kocha wa
Timu hiyo Bw. Bakari Shime ameshukuru Waziri na Watanzania kwa
ujumla kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo na watahakikisha wanapata
ushindi katika mechi ya marudiano kwani wameshayaona mapungufu yaliyojitokeza
na watayafanyia kazi wachezaji watakuwa tayari kuivaa tena Congo Brazavile.
Aidha Nahodha wa Timu hiyo
Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi
kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata maagizo
kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata
ushindi katika mchezo wa marudiano.
“Tunashukuru sana kwa
motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate
ushindi tukiwa ugenini ili tuweze kufuzu” Aliongeza Nahodha Makame.
Timu ya Taifa ya
Tanzania ya vijana chini ya umri wa Miaka kumi na saba
(Serengeti Boys) inayowania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya
Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017
inatakiwa kupata ushindi ili kujihakikishia kufuzu kwa fainali hizo.
No comments:
Post a Comment