Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Rulegea na viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM)wilaya ya Geita wakishiriki kuchimba msingi kwaajili ya Ujenzi wa shule ya Msingi Kijijini Hapo. |
Afisa Elimu wa kata ya Izumacheli Bw Thomson Jerusinga,akisoma taarifa ya Ujenzi wa shule hiyo. |
Diwani wa Kata ya Izumacheli, Bw Ismail Manyama akisisitiza wananchi kushirikiana kwenye shughuli ya Ujenzi wa shule. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisiza wananchi kuwa wamoja na kushirikiana na serikali ili waweze kumaliza ujenzi wa Shule. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herma Kapufi pamoja na wananchi wakishiriki kuchimba Msingi kwaajili ya ujenzi wa shule. |
Katika ujenzi huo wananchi hao wanashirikiana na mkuu wa Wilaya ya Geita
Mwl. Herman Kapufi na viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM).
Hatua hiyo inatokana na wanafunzi kuendelea kupata shida ya kuvuka mara
kwa mara pindi wanapokwenda na kutoka shuleni kwa kutumia mitumbwi hivyo
kuhatarisha maisha yao.
Afisa Elimu wa kata ya Izumacheli Bw Thomson Jerusinga alisema tatizo la
watoto kuvuka maji mara kwa mara limesababisha wananchi wengi kuhama kijijini
hapo.
“Kabla ya tukio la Mei 22 mwaka jana kitongoji
hiki kilikuwa na Kaya 184 lakini baada ya lile tukio la kuzama wanafunzi,
wananchi wengi walihama kwa hiyo ikasababisha kuwepo kwa Kaya 60 badala ya mia
moja themanini na nne(184). Eneo ambalo tunatarajia kuanza ujenzi litaweza
kujenga vyumba vya madarasa pamoja na ofisi za walimu na viwanja vya michezo” Alisema Jerusinga.
Diwani wa Kata hiyo Bw Ismail Manyama alisema wanafunzi wa eneo hilo
wameendelea kupata shida kutokana na kuvuka maji hivyo kukamilika kwa shue hiyo
kutawasaidia kuepuka kwenda kijiji jirani.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi aliwasisitiza wananchi
hao kuwa wamoja ili waweze kufanikisha ujenzi huo wa shule pamoja na Nyumba za
walimu na kwamba serikali ipo nao bega kwa bega kuhakikisha kwamba
wanafanikisha Ujenzi huo.
Nae Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita, Bw Barnabas
Mapande amewataka wananchi hao kutowasikiliza watu wanaowapotosha katika
kushiriki shughuli za maendeleo kwani kufanya hivyo ni kuweka hazina kwa vizazi
vilivyopo na vijavyo.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamesema kuna kila sababu ya kushirikiana
na viongozi wao kujenga shule hiyo kwa manufaa ya watoto wao
No comments:
Post a Comment