Leo September 27 2016 taarifa
iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada wa Milioni
545 kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua
uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Amantius Msole na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda.
Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti
nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia
maafa iitwayo “Kamati Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais
Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika
katika njama za kufungua akaunti hiyo.
Aidha, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai
kutokana na kuhusika katika njama hizo. Hata hivyo Kassim Majaliwa ametoa
wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili
ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya “Kamati Maafa Kagera” ambayo
imetangazwa na Serikali.
No comments:
Post a Comment