Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekutana na wawekezaji wa kampuni
tisa za nchini Korea Kusini na kumuahidi kushirikiana na Serikali ya
Tanzania kuwekeza katika sekta ya kilimo, viwanda, maji, miundombinu, elimu,
afya na michezo.
Wawekezaji hao wanatoka kampuni ya Sima textile, ESM, Jusung
Solar Engineering, Seongnam City FC, Yeong Yang City Korea,Ulsan Vocational
Training, Egis Smart City, MBN
Akizungumza na wawekezaji hao jana jioni (Jumanne, Septemba 27,
2016) kwa niaba ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli, Waziri Mkuu alisema kwamba
Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji ikiwa na fursa za uwekezaji kwenye
sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Licha ya mazingira mazuri ya
uwekezaji pia aliwahahakishia ulinzi kwenye uwekezaji wao.
Waziri Mkuu alisema Korea ya Kusini inashirikiana vizuri na
Tanzania hivyo wanatarajia mengi kutoka nchini huko kupitia wawekezaji hao.
Wawekezaji hao tayari wamefanya mazungumzo na viongozi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijinii Mwanza na kusaini Hati ya
Makubaliano (MoU) kwa ajili ya miradi minne ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya
maji, kiwanda cha nguo, zana kubwa za kilimo na mafunzo ya ufundi.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo, Bw. Son Young Soo alisema
amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza nchini.
Naye, Bw. Jihyun Kim wa kampuni ya Yeong Yang City Korea
ambayo inashughulikia masuala ya kilimo cha mbogamboga alisema watawekeza
kwenye kilimo hususan cha zao la pilipili na watajenga kiwanda kwa ajili
ya usindikaji.
Naye Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee
alisema klabu yake ipo tayari kuwekeza katika shule ya michezo kwa vijana ili
kuongeza kasi ya maendeleo ya soka.
No comments:
Post a Comment