Thursday, 15 September 2016

MKUU WA WILAYA YA GEITA HERMAN KAPUFI AAMURU VIONGOZI WA CHUO CHA UALIMU KUKAMATWA KWA KUSHINDWA KURUDISHA FEDHA

Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi.
 Viongozi hao wameamuriwa kukamatwa baada ya kushindwa kuwarejeshea wanachuo fedha wanazodai kiasi cha shilingi milioni 230.
Hatua ya Kaimu Mkuu wa Mkoa huyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Geita ametoa agizo hilo baada ya chuo hicho kudaiwa kuwadaahili wanachuo wapatao 300 katika kozi ya Early Childhood Development Education (ECDE) kozi ambayo haitambuliki na NACTE.
DC kapufi amesema kwa kipindi chote wanachuo walichokaa chuoni hapo na kupotezewa muda wao ni lazima uongozi uwarudishie vyeti vyao pamoja na fedha walizolipa.

Awali Kaimu Mkurugezi wa chuo hicho aliomba kulipa kiasi cha shilingi milioni 115 kati ya fedha hizo jambo ambalo lilikataliwa na wanachuo pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa.
Sakata hilo limeanza mapema mwezi huu baada ya wanachuo hao kugoma kuingia madarasani wakishinikiza uongozi ulipe fedha zao wanazodai ingawa kumekuwepo na mvutano mkali baina ya mkurugenzi wa chuo na aliyekuwa mkuu wa chuo hicho.

Mkuu wa chuo anatuhumiwa kupokea ada na kuwadahili baadhi ya wanachuo bila mmiliki wa chuo hicho Bwana Richard Mchele kushirikishwa kutambua kuwepo kwa udahili wa wanafunzi wasio na sifa ulikuwa ukiendelea huku mmiliki akiwa hajui chochote.

No comments:

Post a Comment