Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mafunzo ya ununuzi wa hisa ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa maarifa ya Nyumbani Mjini Geita. |
Meneja Mahusiano ya Umma wa CMSA Bw Charles Shirima akifundisha namna ya uwekezaji wa hisa. |
Serikali kupitia
mamlaka ya masoko ya dhamana na mitaji nchini ya Capital Markert and Securities
Authority, CMSA imesema ununuzi na uuzaji wa hisa na Hati fungani za makampuni
na serikali ni mbinu nzuri za kujiwekea akiba na kumfanya mtu kutajirika.
Amesema wajasiriamali
na wananchi kwa ujumla wakiwa na tabia ya kuweka akiba kwa kununua Hisa za
makampuni mbalimbali ya kibiashara wanaweza kupata utajiri kwa njia ya kupata
gawio kila mwaka baada ya kampuni husika kupata faida na kugawa faida kwa
Wanahisa wake.
Ametaja baadhi ya
makampuni amabayo yanafanya vizuri zaidi hadi sasa kwenye soko la Hisa na kutoa
gawio la faidi kwa wanahisa wake kuwa ni pamoja na Tanzania Breweries
Limited(TBL),TOL Gases Limited,NMB Bank,CRDB Bank,Tanzania Tea Packers
Limited,Tanzania Cigarette Company naTanga Cement Company Limited.
Amesema, mbali na
gawio la faida ya kila mwisho wa mwaka baada ya kampuni kupata faida,mmiliki wa
Hisa anaweza kuuza hisa zake muda wowote na kupata faida baada ya kugundua kuwa
kipindi hicho Hisa za kampuni hiyo zimepanda bei kwenye soko la hisa.
Akifunga mafunzo hayo
Kiongozi kutoka kwenye Taasisi ya maendeleo ya vijana na ushirikiano Tanzania
Aloyce Masana,aliishukuru sana CMSA kwa kutoa mafunzo hayo kwani wafanya
biashara wengi walikuwa hawajui kama Hisa na Hati fungani ni uatijiri
uliofichika.
No comments:
Post a Comment