Halmashauri ya wilaya ya Geita imefanikiwa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu 131,445 kwa uwiano wa chandarua kimoja kwa watu wawili kwa jumla ya kaya 467,609 katika harakati za kutokomeza ugonjwa wa malaria ambao bado ni tishio kwa eneo la kanda ya ziwa.
Utafiti wa malaria uliofanyika mwezi Oktoba, 2017 katika shule 5 za
Msingi Halmashauri ya wilaya Geita unaonyesha wanafunzi
396 kati ya 674 sawa na asilimia 58.8%ya wanafunzi waliopimwa waligundulika na
vimelea vya Malaria hali iliyopelekea Halmashauri kuja na mkakati
mwingine wa kuhakikisha vyandarua vyenye viwatilifu vinagawiwa
shuleni na pia watoto wanafundishwa mbinu mbalimbali za kupambana
na Malaria.
Mwaipaja ameeleza kiwango cha upimaji wa malaria kimeongezeka
kutoka asilimia 91.8% mwaka 2016 hadi asilimia 98.8% mwaka
2017 na watu waliogundulika wana malaria walipatiwa tiba.
Akilezea Sababu zinazochochea maambukizi ya malaria katika jamii ni
pamoja na tabia ya jamii kuchelewa kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za
afya kwa ajili ya utambuzi na kupata tiba ya malaria, Kutumia dawa bila kupima,
kutokamilisha dozi kwa wagonjwa wa malaria, Matumizi yasiyo rasmi ya
vyandarua kwa shughuli zisizokusudiwa pamoja na Kugomea shughuli za
unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani”.
“Katika kuhakikisha Malaria inaondoka kabisa Geita kwa sasa tunatoa elimu
kwa jamii na tunahakikisha matumizi salama na sahihi ya vyandarua yanatelekezwa
na ndio maana tumeamua kugawa vyandarua hivyo kwenye ngazi za shule za msingi
kama njia mojawapo ya kuzuia malaria” Ameongeza Mwaipaja.
Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
baina ya Wataalam kutoka Halmashauri ya wilaya ya Geita pamoja na
mashirika yasiyo ya kiserikali ya “Tanzania Communication and Development
Center”(TCDC),Pamoja na New Light Children Organisation (NELICO) kwa
lengo la kutathimini hali ya Ugonjwa wa Malaria wilayani hapa.
No comments:
Post a Comment