Tayari Rais Dr John Magufuli ameshatoa kwa idara hiyo Sh bilioni 10
na kwamba ujenzi wa ofisi hizo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza wakati alipotembelea ofisi hizo
leo, Dr Mwigulu amemshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kuwapa fedha hizo ambzo ni Sh
bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi makao makuu ya Uhamiaji.
Amesema tayari kwasasa eneo kubwa lenye mita
za mraba 9,777 limepatikana kwa ajili ya kujenga jengo kubwa na la kisasa kwa
idara hiyo.
"Eneo limeshapatika kubwa la kutosha la
kujenga ofisi ya kisasa kama ambavyo muheshimiwa Rais amesemea wakati
anatuhaidi kutupa fedha hizi sasa tumepata eneo la kutosha ambalo lipo
karibu na ofisi zote muhimu kama vitambulisho vya Taifa,zimamoto na ofisi
zingine za serikali ambapo itasaidia kama mtu akifika uhamiaji anaweza kupata
zingine ambazo zipo karibu". Aliongeza
waziri mwigulu.
Waziri mwigulu ametoa rai kwa idara ya uhamiaji
kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani kuchapa kazi kwao ndio kumefanya wao
kupata fedha hizo za ujenzi kwa haraka na fedha za kununua nyumba za makazi ya
askari Dodoma kwani kama wangefata kupata fedha katika bajeti ya wizara
ingechukua mda mrefu kupatikana fedha hizo hivyo kufanya kazi kwao vizuri kunamfanya
hata yeye kuwa waziri wa mamboya ndani mzuri.
Naye, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dr Anna
Makakala amemshukuru muheshimiwa Rais Dr John magufuli kwa kuwapa fedha
hizo kujenga jengo la kisasa na mpaka sasa wameshapa eneo kubwa kabisa ambalo
litawawezesha kupata mahitaji yote.
"Sisi kama idara tunajukumu la kufata
taratibu zote kwa haraka iwezeka nanvyo ili jengo hili ndani ya mwaka wa fedha
ujao liweze kukamilika kwasababu kama fedha ni zipo", alisema Dr Anna.
No comments:
Post a Comment