Choo cha wanafunzi ambacho kinamatundu matatu na kinatumiwa na wanafunzi 2072 shuleni hapo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mchongomani kata ya
Katoro mkaoni Geita wanasomea nje wakiwa wamekaa chini na wengine
kubanana kwenye madawati kutokana na shule hiyo kukabiliwa na Upungufu wa
madawati na vyumba vya madarasa.
Baadhi ya wanafunzi hao Jesca Michael na Hoja Hassan
wamesema hali hiyo imekuwa ikisababisha utoro kwa baadhi ya wanafunzi na
kwamba mvua zinaponyesha wamekuwa wakisitisha masomo.
“Tumekuwa tukipata shida kubwa sanaa kusomea
nje hali hii imekuwa ikisababisha baadhi ya wanafunzi wenzetu kushindwa kuja
shule kutokana na haya mazingira ya kusomea nje” Alisema Jesca.
“Tunaathirika
sanaa macho kusomea nje kwani muda mwingine jua likiwa kali limekuwa
likituumiza macho na siku nyingine mvua zikinyesha uwa tunashindwa kusoma hali
hii imekuwa ikisababisha kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yetu tunaomba
serikali itusaidie kwani tunateseka sanaa hadi muda mwingine tunawaonea huruma
walimu wetu." Alisema Hoja.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw
Faustine Makulu amekili kuwepo kwa tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa
na kwamba uhitaji wa vyumba vya madarasa ni 46 na kwasasa wamejenga vyumba 4 na
vinavyotumika ni viwili huku wanafunzi waliopo shuleni hapo ni 2072.
“Hapa shuleni kwangu hali siyo nzuri pamoja na
jithada ambazo zimeendelea kufanywa na serikali lakini uhitaji ni mkubwa sanaa
ukilinganisha na watoto waliopo na madarasa ambayo yapo utaona hali ilivyo
kiuweli hadi sasa hivi jitihada ambazo zinaendelea ni ujenzi wa vyumba vitatu
vya madarasa”Alisema Mwalimu Makulu.
Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Geita,
Bw Ali Kidwaka alisema wanafanya jitihada za kujenga vyumba vya madarasa
322 wilayani humo vikiwemo katika shule hiyo na kwamba wanatarajia kufikia
Desemba mwaka huu wawe wamepunguza changamoto ya upungufu wa madarasa.
|
No comments:
Post a Comment