Serikali kupitia Shirika la Viwango nchini, TBS limetakiwa kuchunguza
kemikali bandia zinazouzwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kwa
wachimbaji wadogo wa madini hali inayosababisha hasara kwa wachimbaji hao.
Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA) Bw
John Bina amesema hayo baada ya kikao kilichowakutanisha wachimbaji wadogo
Mkoani Geita kwa lengo la kujadili namna Serikali inavyoweza kufanikisha ujenzi
wa soko la madini kwa kanda ya ziwa.
Alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza
kemikali bandia kwa wachimbaji wadogo na hivyo kuwasababishia
hasara.
“Tunaomba serikali na TBS kuangalia sanaa haya madawa ambayo
yanaingia nchini kuhakikisha wanachunguza kemikali hizi kwani kwa sasa
uzalishaji unashuka kwa kiasi kikubwa wa madini ,na nyie wachimbaji niwaombe
muwe mnachunguza kabla ya kununua kwani kweli mnaingia hasara kubwa sanaa” Alisisitiza Bina.
Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Bw Nuru
Shabani alisema kwa kuuziwa Kemikali hizo bandia amekuwa akiathirika
katika shughuli zake.
“Kiukweli tunaathirika sanaa na hili halina ubisha sasa hivi
unaweza kununua tani moja ya kaboni unakuta inapitisha bila ya kushika mali
inamaana hadi iwe na pipim kuanzia mia saba hadi mia nane ,Ila kwa sasa
nashukuru walau serikali imetambua mchango wetu na imetuthamini mimi nilikuwa
naomba kupitia Kitengo chetu tuwe na wasimamizi ambao watatusaidia kubaini
kemikali hizi” Alisema Nuru.
Bw John Bina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia kero za
wachimbaji wadogo alisema pamoja na matatizo hayo lakini wachimbaji
hao wamekubaliana kuanzishwa kwa soko la madini Mkoani Mwanza ili kudhibiti
vitendo vya utoroshwaji wa madini.
No comments:
Post a Comment