Rais John Magufuli
amesema ujenzi wa reli ya kisasa nchini utatoa ajira za moja kwa moja 30,000 na
zisizo za moja kwa moja 600,000.
Akizungumza leo
Jumatano Machi 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo kutoka
Makutopora mkoani Dodoma hadi Morogoro, Rais Magufuli amesema mbali na kutoa
ajira, ujenzi huo ukikamilika utanyanyua uchumi wa nchi.
“Ujenzi wa reli hii
utasaidia kutunza barabara zetu kama mnavyojua nchi yetu imepinga hatua katika
ujenzi wa barabara. Barabara zetu hazidumu kutokana na kubeba mizigo mizito
ambayo inaweza kusafirishwa kwa njia ya reli,” amesema.
“Uwapo wa reli hii
utapunguza gharama za ukarabati wa barabara zetu. Ujenzi wa reli hii utatoa
ajira za moja kwa moja 30,000 na zisizo za moja kwa moja 600,000… juzi
tuliambiwa sasa tumefikia watu milioni 55, watu wanasema kwa nini tunazaliana,
mimi nasema tuazaliane tu. Mnapokuwa wengi mnakuwa na sauti. Katika jumuiya
tulizopo sisi tupo wengi tuna sauti, jambo la msingi tuchape kazi,” amesema.
Amewataka
Watanzania kuacha kuogopa wingi wao na kwamba, jambo la muhimu ni kufanya
kazi.
“Denmark ina watu
milioni tano lakini wakati mwingine inatoa msaada hata kwa nchi kama Tanzania
kwa sababu watu wake wanafanya kazi. Nchi nyingi duniani zimeshindwa duniani
kwa sababu zinakopa halafu zinapewa masharti magumu. Sisi tumejenga kwa hela
ndogo tofauti na ilivyotarajiwa,” amesema.
No comments:
Post a Comment