Thursday, 29 March 2018

UHABA WA VYOO SHULE YA SEKONDARI LUBEMBELA WAWALIZA WANAFUNZI




Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lulembela iliyopo kata ya Lulembela Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita wanalazimika kukimbilia vichakani kwenda kupata huduma ya choo kutokana na shule hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo.

Shule hiyo   yenye jumla ya wanafunzi  658, wanalazimika kutumia matundu sita  ya vyoo  huku yakiwa yamejaa kwa uchafu  na miundombinu yake ikiwa ni mibovu na ambayo hairidhishi  jambo linalopelekea kukosekana kwa vyoo safi na salama.

Baadhi ya wanafunzi akiwemo Rashidi Hassani na Elfida Msebi wamebainisha kero hizo, huku Mkuu wa shule hiyo Ernest Mganga akikiri kuwepo kwa changamoto ya vyoo.

No comments:

Post a Comment