Jeshi la polisi
mkoani Geita , limewataka wananchi katika kuelekea siku
kuu ya pasaka pamoja na uzinduzi wa mwenge Kitaifa, kujiepusha na vitendo vya
uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na wazazi kuhakikisha usalama na watoto
wanapokuwa kwenye maeneo ya barabara na mitaani.
“Niseme tu kwamba
tumejipanga vya kutosha kuhakikisha kila sehemu inakuwa salama na pia niwaombe
watu kusherekea kwa amani siku kuu ya pasaka na kwa Yule ambaye hataonekana
kutaka kuvunja amani sheria kali zitachukuliwa dhidi yake”Alisema Kamanda
Mponjoli.
Kamanda Mponjoli pia
amewata wazazi na walenzi kuwa makini na watoto wao na kuhakikisha wanawachunga
kwenye kipindi cha siku kuu huku akipiga vita suala la disko toto.
Sanjali na hayo
Kamanda Mponjoli, amewatahadharisha watu ambao wamepanga kuandamana tarehe
26 april kuachana mara moja na suala hilo na kwamba wamejipanga vyema kulinda
amani ya Mkoa na mtu yeyote ambaye atabainika hatua kali zitachukuliwa dhidi
yake.
No comments:
Post a Comment