Mdhibiti na Mkaguzi
mkuu wa hesabu za serikali Profesa. Mussa Assad ameomba radhi wananchi na
serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya
kimatamshi, deni hilo ni himilivu.
Profesa Assad ametoa
taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema deni halisi ni shilingi trillion 46.08
na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi na
taasisi za serikali.
CAG wakati akitoa
ripoti hiyo kwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu suala la muenendo wa deni la
taifa alidai kuwa deni la taifa si himilivu lakini kwa mujibu wa utafiti ambao
wamefanya wao CAG ameibuka na kuomba radhi na kusisitiza kuwa ripoti ya CAG ni
siri hadi itakapowasilishwa bungeni.
No comments:
Post a Comment