Nyumba ikiwa imeenea maji kutokana na kifusi ambacho kimelalamikiwa na wananchi.
Wananchi waishio Mtaa wa Katundu Kata ya Kalangalala Mkoani Geita
wamemlalamikia mkandarasi ambaye anajenga Barabara ya Kilomita 1.2 inayotoka
Amerikani Chips kuelekea Jimboni kuweka kifusi cha mchanga hali
ambayo imekuwa ikisababisha maji kuelekea kwenye makazi yao pindi mvua
zinaponyesha.
Mkandarasi huyo ambaye anajulikana kwa jina la Nyakiling’ani
Constraction Limited(NCL) anatekeleza mradi huo kwa ufadhili wa Benki ya
dunia na kusimamiwa na halmashauri ya Mji wa Geita.
Akizungumza na Mtandao huu, Bi,Getruda Daudi alisema wameendelea kupata
shida kubwa kutokana na mkandarasi huyo kuweka kifusi na pindi wanapomwambia
amekuwa akiwaambia hana gharama za kukitoa kifusi hicho.
“Mvua zikinyesha tumekuwa tukipata shida sanaa jamani yani maji yote
yanakuja kwenye nyumba zetu na sababu ni hiki kifusi ambacho mkandarasi amegoma
kukitoa tumekwisha mwambia hadi na diwani wetu lakini alikuja akapiga picha
akaondoka na sisi ndio tunaopata shida ila tunaona yuko kimya hatujui
tufanyeje” Alisema Bi. Getruda.
Hata hivyo kwa upande wake Bw, Nzugila
Mazoya pia amelalamika kitendo cha mkandarasi wa eneo hilo kuchukua muda
mrefu bila ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo pamoja na daraja hali ambayo
kwa sasa imekuwa ikiwapa shida kwa kuzunguka umbali mrefu kutokana na njia
kuzibwa.
Sanjari na hayo baadhi ya wafanyakazi ambao wanafanyakazi na Kampuni hiyo
akiwemo Lanslaus Joseph na Majura Mfungo wamelalamikia kutokulipwa
mishahara kwa muda mrefu sasa na pindi wanapomuuliza msimamizi amekuwa
akiwasisitiza kufanya kazi kwa madai kuwa pesa itakuja na kwamba hawaoni
jitihada ambazo zinafanyika za malipo hadi sasa.
Kutokana na madai hayo , Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Mji
kuhakikisha anaisimamia Kampuni ya Nyakiling’ani ikiwa ni pamoja na
kukatwa fedha kutokana na wananchi ambao wanaishi mitaa ya Katundu kujitolea
kuondoa kifusi hicho.
“Mtaro umejengwa mwaka umefika kifusi kile kimekuwa ni mlima na kero kwa
wananchi ,wananchi wale wanakwenda kuondoa kifusi hicho sasa ni wito wangu
mkateni huyo mkandarasi maana ni ndani ya mkataba wake” Alisema Luhumbi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji mhandisi Modest Apolinary alisema
amebaini kuwa kampuni hiyo ina uwezo mdogo wa kutekeleza mradi na
kwamba imewekwa kwenye uangalizi baada ya muda wa utekelezaji
kuisha.
Kufuatia Malalamiko hayo ya wananchi msemaji wa kampuni hiyo
Bw, Raulent Mwita kwa Njia ya simu ambapo ameeleza kuwa waliweka tuta
kifusi hicho kutokana na ujenzi ambao wanaendelea nao kwa sasa na suala la mvua
namna lilivyokuwa likikwamisha ujenzi.
No comments:
Post a Comment