Maandamano ya wanawake wakielekea katika dhifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe. |
Baadhi ya wakina mama wakionesha mabango ambayo walikuwa wamebeba wakati wa maandamano mbele ya mgeni Rasmi. |
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake,akikagua baadhi ya bidhaa ambazo zimetengenezwa na wakina mama wajasiriamali. |
Chimbuko la Siku ya Wanawake Duniani lilianza miaka mingi na mwaka 1911,
baada ya Wanawake nchini Marekani kuandamana kudai haki zao ambazo walikuwa
wakizikosa: kama vile kulipwa ujira mdogo, kufanyishwa kazi ngumu na kwa masaa mengi,
kukosekana kwa huduma za jamii na ubaguzi wa kijinsia.
Kila mwaka maadhimisho haya yanafanyika na kubainisha changamoto
mbalimbali zinazowakabili wanawake na kuwa kikwazo kikubwa cha kusonga mbele
katika kujikwamua kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.
Mkoani Geita maadhimisho haya yamefanyika wilayani Bukombe,huku
yakiuzuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo
Mhandisi , Robert Luhumbi pamoja na Naibu waziri wa madini ambaye pia ni mbunge
wa Jimbo hilo Doto Biteko.
Mkuu wa mkoa huo ambaye alikuwa ni mgeni rasimi ametumia nafasi hiyo
kuvitaka vyombo vya habari kuendelea kuibua na kutangaza vitendo vya
ukatili ambavyo vimekuwa vikifanywa dhidi ya wanawake na watoto
ndani ya jamii.
“Vyombo vya habari wakiwa ndio
wadau wakuu wa kuibua masuala mbali mbali yasiyo ya haki ndani ya jamii ,kwa
kushirikiana na serikali na jamii yote ,ushirikiano wenu wa dhati wa kusaidia
kuibua vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ndani ya jamii,una umuhimu
mkubwa .Pia niwasihi Jeshi la polisi ,kuimarisha madawati ya jisnia na watoto
kwenye vituo vya Polisi na kushirikiana kikamilifu na wadau wa harakati za
kuwakomboa wanawake na watoto kwa ajili ya kusaidia kupokea ,kufuatilia na
kushughulikia kesi za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa uharaka zaidi”
Alisema Luhumbi.
Akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa jukwaa la
wanawake Wilayani humo,Bi Leticia Mourice alisema maendeleo ya wanawake katika
Nyanja mbali mbali hapa nchini ,yamekuwa yakikwamishwa na nafasi ambazo wanazo
wanawake kama wazazi walezi na wafanyakazi.
“Kwa upande mwingine ,mila na desturi
kandamizi kwa baadhi ya maeneo ,zimeendelea kujengwa na kukuzwa.Jambo hili
limeleteleza kutokuwepo na usawa kwa Jinsia katika Sekta zote za maendeleo
hususani katika Nyanja ya elimu,ajira,afya,umiliki wa rasilimali ardhi,urithi
na ushirikishwaji katika ngazi mbali mbali za maamuzi” Alisema Bi. Leticia,
Siku ya wanawake Duniani imepambwa na kauli mbiu isemayo” Kuelekea uchumi
wa viwanda, tuimalishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake
vijijini"
No comments:
Post a Comment