Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Nyakabale wilayani Geita wametelekeza mwili wa marehemu nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa huu, Elias Ndarawa.
Wananchi hao waliubeba
mwili wa Zacharia na kuulaza kwenye kitanda cha mwenyekiti huyo.
Majaliwa Shaban ambaye
ni ndugu wa marehemu Zacharia amesema leo Machi 12,2018 kwamba nduguye alipigwa
Machi 5,2018 akiwa eneo la Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM) akiokota mabaki ya mawe
ya dhahabu maarufu magwangala.
Amesema Zacharia
alipelekwa polisi alikokaa kwa siku sita na aliporudi uraiani hali yake ilikuwa
mbaya.
Majaliwa amesema
nduguye alipelekwa hospitali alikofariki dunia Jumamosi Machi 10,2018 na hadi
sasa hakuna kiongozi aliyefika kwenye msiba huo wala kutoa kauli yoyote.
Mkazi wa mtaa huo,
Johnson John amesema hawapo tayari kuzika hadi Serikali itakapotoa kauli kuhusu
hatima ya maisha yao kwa kuwa polisi jamii wamekuwa wakiwapiga na kuwajeruhi.
Jana, Machi 11,2018
wananchi walivamia eneo la kituo cha polisi jamii kilichopo mtaa wa Manga na
kukichoma moto kwa madai kwamba wamempiga na kumuua Zacharia
No comments:
Post a Comment