Mazungumzo kati ya
Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza rasmi leo tarehe 12 Machi, 2018
Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo
kamati iliyoundwa na Mhe. Rais Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na
Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na
Mwanasheria Mkuu wake Bw. Mukesh Bhavnani.
Mazungumzo hayo
yanalengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili
(Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel) na kuimarisha sekta ya mawasiliano
nchini Tanzania.
Kampuni ya Bharti
Airtel iliomba kufanyika kwa mazaungumzo hayo baada ya kamati iliyofanya
uchunguzi kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania kuwasilisha ripoti yake
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Machi, 2018
No comments:
Post a Comment