Gari aina
ya lori lenye namba za usajili T415 DJG limechomwa moto
baada ya kumgonga mwendesha pikipiki na
kusababisha kifo cha Matha Paulo aliyekuwa ni Muuguzi wa
kituo cha afya cha Kaseme Wilayani Geita alikuwa amebebwa kwenye pikipiki hiyo.
Tukio hilo limetokea
majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Kasesa kwenye barabara ya
katoro-Lunzewe ambapo mwendesha boda boda na abiria wake walikuwa wakitokea mji
mdogo wa Katoro,huku watoto wawili kikiwepo kichanga cha miezi miwili waliokuwa
wamepakatwa na marehemu mama yao wakinusulika kifo.
Akisimulia shuhuda
wa tukio hilo Bw,Mayala Bushibe, amesema yeye alikuwa ameongozana na bodaboda
iliyopata ajali,huku nyuma na mbele yao yalikuwapo magali mawili likiwemo lori
yakipishana na boda boda alipojaribu kulipita ndiyo likawagonga gari hilo.
Josia Thobias ambaye
ni mkazi wa Kaseme na Tarafa Maganga wamesema tukio la
namna hiyo sio la mala ya kwanza kutokea kwani ajali za hivyo
zimeendelea kujitokeza na kwamba ni mala ya pili kutokea.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Geita Mponjoli mwambulambo amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa pikipiki ambaye alikimbia
baada ya kutokea kwa ajali,huku akiwataka wananchi kuachana na vitendo vya
kujichukulia sheria mkononi.
No comments:
Post a Comment