Wednesday 28 March 2018

VIONGOZI WA KIKRISTO MKOANI GEITA WAHIMIZA AMANI NA UTULIVU KWENYE PASAKA

Image result for KANISA


Baadhi ya Viongozi wa Kikristo mkoani Geita wamewataka Wakristo kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa amani na utulivu na kujiepusha na matendo maovu wakati wa sherehe hizo.

Padri Gerald Singu ambaye ni Paroko wa Parokia ya Bikra Maria wa Fatima Geita, Mchungaji Gerson Yoboka ambaye ni kiongozi mkuu wa kanisa Anglikana mkoani Geita na Mchungaji Mathias Michael Kasente wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, KKKT Usharika wa Upendo wametoa kauli hiyo walipokuwa wakitoa ujumbe wao wa Pasaka kwa Waamini.

Wamesema ni vema Wakristo wakabadilika na kuacha dhambi badala yake wafanye mambo ya kumpendeza Mungu na kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakipania kufanya matendo maovu katika Sikukuu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment