Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la chama
cha mapinduzi Ccm lililopo kata ya katoro Mkoani Geita wamekiomba chama hicho
kuwajengea choo bora kwakuwa kilichopo kwasasa hakikidhi mahitaji ukilinganisha
na idadi ya watu wanao ingia na kutoka ndani ya soko hilo.
Wakizungumza na storm habari baadhi ya wafanya
biashara hao Samweli Jaksoni, Milanga Shukuru na
Paulina Petro katika soko hilo wamesema wanapata wakati mgumu pindi
wanapo hitaji huduma hiyo kwani choo kilichopo kwasasa nikidogo ukilinganisha
na idadi ya watu kwenye soko hilo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara katika soko
hilo Bw Charles Mlale amesema choo kilichopo kwa sasa siyo
bora na kina idadi ya matundu manne hali inayo walazimu kwenda katika kaya
jirani kuomba huduma ya kujisaidia.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya
ukusanyaji wa fedha wa chama cha mapinduzi Ccm kwenye soko hilo Bw
Majaliwa Bukeke amekili kuwepo kwa changamoto hiyo nakusema kuwa wapo
mbioni kutafuta mzabuni watakae ingia nae mkataba ikiwemo kujenga choo cha
kisasa katika soko hilo.
No comments:
Post a Comment