Monday 19 March 2018

WATU 12 WAMEKAMATWA MKOANI GEITA KWA KUUZA VIUADUDU KINYUME CHA SHERIA

Dawa za kuuwa wadudu wa Pamba.

Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mkoa.

Baadhi ya wakuu wa idara na wakurugenzi wakiwa kwenye Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwasisitiza wakurugenzi na wakuu wa idara mbali mbali kufanya kazi kwa Weledi.
Serikali mkoani Geita imekamata dawa za viuadudu 428 vilivyotakiwa kupelekwa kwa wakulima wa pamba vijijini badala yake vikapelekwa kwenye maduka ya kilimo kinyume na matarajio ya serikali.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu wadau wa zao la pamba walipokutana kujadili kilimo hicho.

Akizungumza na wakurugenzi na wakuu wa idara wa halmashauri za mkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Luhumbi alisema hadi sasa wanawashikilia watuhumiwa 12 wanaotoka  kwenye halmashauri  za Chato , Geita DC na Geita mji.

Tumegundua viuadudu mia nne ishirini na nane(428) vilivyotakiwa viingie vijijini kwa wakulima vimeingia kwa mawakala kwenye maduka ya pembejeo kinyume na taratibu, mwongozo na  mpango uliokusudiwa kwa hiyo watuhumiwa 12 tayari wamekamatwa katika Wilaya mbili, wilaya ya Chato tumepata viuadudu tisini na sita(96), Geita Mji tisini na nane (98)na kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita tumepata mia mbili thelasini na Nne (234)” Alisema Luhumbi.

Hata hivyo Mhandisi Luhumbi ameiagiza TAKUKURU pamoja na vyombo vya dola kuwakamata wote waliohusika na usambazaji wa dawa hizo vikiwemo na vikosi kazi ngazi ya kijiji kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kamanda wa Takukuru mkoani Geita Bw Thobias Ndaro alisema wanaendesha msako kuwabaini wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo kwenye maduka.

No comments:

Post a Comment